fbpx
Huawei, simu, Uchambuzi

Hii hapa Huawei GR5 2017; Simu janja mpya kutoka Huawei kwa mwaka 2017 #Uchambuzi

huawei-gr5-simu-janja-2017
Sambaza

Simu janja ambapo kila uchwao basi inatoka mpya/toleo jipya lililo bora kuliko toleo lililopita vivyo hivyo Huawei nao wameamua kutoa kilicho bora na ambacho kwa hakika utakipenda na kujipanga kuweza kumiliki simu janja mpya kutoka Huawei.

Katika orodha ya makampuni ambayo yanaleta ushindani katika soko la simu janja basi Huawei ni moja ya kampuni hizo na huko Australia Huawei (kampuni) inashikilia nafasi ya tatu nyuma ya Apple na Samsung. Kwanini TeknoKona tunasema utaipenda simu  hii?

Sifa za Huawei GR5 2017

Simu hii ambayo kwa kiasi kikubwa ni maboresho ya Honor 6X ina mengi mazuri hasa hasa kwa wale ambao uwezo wa kununua simu kwa bei ya juu sana inakuwa ni changamoto.

  • Kioo. Kioo cha simu janja hii kina ukubwa wa 5.5″, LTPS IPS LCD, 1980 x 1020, 403ppi huku uwiano kati ya kioo na umbo la simu ukiwa ni 71.8%.
  • Programu endeshaji. Inatumia Android: 6.01 plus EMUI4.1. Pia utaweza kuboresha na kutumia Android Nougat Q2.
  • Prosesa. Raha ya simu/kompyuta iwe na prosesa kubwa kuweza kufanya vitu vingi ndani ya muda mfupi. Huawei GR5 ina prosesa nane aina ya Kirin 655, kasi yake ikiwa ni 4 x 2.1GHz na 4 x 1.7GHz.
  • RAM na diski uhifadhi. Ina RAM GB 3 na uwezo wa kuhifadhi vitu vyenye ukubwa wa GB 32, bila kusahau ina kubali diski hifadhi ya ziada (memory card) ya mpaka GB 256. Inatumia laini 2.
  • Betri. Betri yake ina uwezo wa 3340mAh, ndani ya saa mbili na nusu betri inakuwa tayari imeshajaa. Pia inakubali teknolojia ya OTG.
    Huawei GR5 2017 kwenye masuala ya intaneti inakubali teknolojia ya Cat 6, 300/50Mbps na uzito wake ukiwa 150.9 x 76.2 x 8.2 mm x 162g.

    Sifa kuu ya Huawei GR5 2017 ni kwamba ina kamera mbili za nyuma lakini pia ikipatikana kwa bei chee kabisa ya $399 (zaidi ya Tsh. 877,800) ukilinganisha na simu janja nyingine kutoka makapuni nguli zinzoanzia kati ya $500 mpaka $799.

Soma pia: Simu ya Honor kutoka Huawei

INAYOHUSIANA  Simu Janja Mpya Kutoka Infinix: Jua Sifa Za Infinix S5!

Sifa nyinginezo

Kamera ya mbele ina 8MP, kurekodi picha jongefu (video) zenye ubora wa 1080. Kamera ya nyuma ina lensi mbili za 12MP+2MP huku sensor zake zikiwa na ukubwa wa 1/2.9″. Ina teknolojia ya Wi-Fi N, Wi-Di, Bluetooth 4.1pamoja kufungua kwa kutumia alama ya kidole (fingerprint sensor). Bila kusahau ina redio na inatumia teknolojia ya  DTS na ANC microphones.

Kwa hakika ni simu inayovutia na ina mengi mazuri katika kulta ushindani katika soko la simu janja. Uamuzi ni wako kwenda kununua simu ya milioni na ushee au ununue Huawei GR5 2017. Tuandikie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: iTwire, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|