fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Intaneti Maujanja Mtandao wa Kijamii simu Teknolojia TikTok

TikTok yaongeza vipengele vya mapato kwa watengeneza maudhui, ikijumuisha vidokezo na zawadi za video

TikTok yaongeza vipengele vya mapato kwa watengeneza maudhui, ikijumuisha vidokezo na zawadi za video
Spread the love

TikTok leo imeleta njia mpya kwa waandaaji wa maudhui kupata pesa kupitia maudhui yao. Ingawa tayari jukwaa hili la video fupi liliruhusu wataarishaji wa maudhui kukubali zawadi pepe kutoka kwa mashabiki wakati wa video za mbashara TikTok. Seti hii ya vipengele vipya itawaruhusu wataarisha maudhui kukubali malipo na zawadi wakati hawafanyi mbashara kupitia nyongeza ya vidokezo na zawadi za Video.

Vipengele hivi vinatolewa pamoja na tovuti mpya ya “Creator Next”, ambayo hupanga fursa zote za mapato za TikTok katika sehemu moja. Kampuni hii pia inapanua ufikiaji wa Soko lake la Watengeneza maudhui lililozinduliwa mwaka 2019 ambalo husaidia makampuni mbalimbali kuungana na waandaa maudhui yanayofadhiliwa na video za mapendekezo. Sasa watengeneza maudhui wa TikTok walio na angalau wafuasi 10,000 wataweza kujiandikisha kwenye Soko la Watengeneza Maudhui la TikTok ili kushirikiana na makampuni kwenye fursa mbalimbali.

SOMA PIA  Nougat: Android 'N' imepata Jina!

Wakati huo huo, kipengele cha kudokeza na kutoa zawadi za video kitaruhusu wataarisha maudhui kuchuma pesa kutokana na video zao huku wakitoa njia kwa mashabiki waonyeshe msaada wao kwa watengeneza maudhui wanaowapenda kwa njia mpya. Kwa pamoja, vipengele hivi vinaiweka TikTok katika ushindani wa moja kwa moja na majukwaa mengine ya mitandao ya kijamii, kama vile Instagram au YouTube, ambapo watengeneza maudhui wana njia mbalimbali za kupata mapato kutokana na maudhui yao.

watengeneza maudhui

Picha: Muonekano wa App ya TikTok

Tovuti ya Mtandaoni ya Creator Next pia huunganisha watayarishaji kwenye fursa nyingine nyingi za mapato, ikiwa ni pamoja na Soko la Wataarisha maudhui na Hazina ya Waandaa maudhui ya TikTok, ambayo huwalipa wataarishaji moja kwa moja kwa maudhui maarufu.

SOMA PIA  Matoleo ya Kompyuta mpakato (Laptop) za HP za mwaka 2021 na sifa zake

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake pamoja na kupata habari za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania