fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Samsung simu

Huenda mwisho wa simu janja za Samsung Galaxy Note sasa umefika

Huenda mwisho wa simu janja za Samsung Galaxy Note sasa umefika
Spread the love

Ni miaka 10 na zaidi ya mwezi mmoja (Oktoba 2011-leo) tangu simu janja ya kwanza kutoka familia ya Samsung Galaxy Note itoke na kufungua ukurasa mpya wa ingizo jipya kwenye soko la rununu kutoka kwa kampuni hiyo yenye makao yake makkuu Korea ya Kusini.

Mapema mwaka huu zilikuwepo taarifa kuwa hatutaona toleo jipya la simu janja Samsung Galaxy Note na badala yake watatoa rununu nyingine kwa maana ya kwamba kuwekwa “Kiporo” hadi mwakani kwa simu hizo ambazo katika kipindi cha muongo mmoja zilikumbana misukosuko mbalimbali ambayo kwa hakika iliyumbisha na kushusha heshima ya kampuni duniani kote.

SOMA PIA  Apple kubadilisha baadhi ya betri katika iPhone 6S zinazojizima zenyewe

Kwa taarifa zilizopo zinasema kuwa huenda toleo la rununu kutoka Samsung Galaxy Note limekia mwisho kwani simu janja hizo hazijaonekana kabisa kwenye mpango wa kutoka mwaka 2022! Na nguvu kubwa huenda ikiwekwa zaidi kwenye zile zinazoweka kukunjika/kukunjuka (Galaxy Flip & Fold).

SOMA PIA  Samsung inatengenza vioo vya OLED kwa ajili ya simu janja za iPhone 13 Pro

Kati ya mwaka 2019-20 Samsung Galaxy 10 (ya kulia pichani) karibu 12.7 milioni na Galaxy Note 20 (ya kushoto pichani) milioni 9.7 tu ndio ziliozika huku Galaxy Z Flip pekee ziliuzwa rununu milioni 13+.

mwisho wa simu

Kufikia mwisho wa simu janja za Samsung Galaxy Note huenda kukawa kumechagizwa na mauzo.

Ni wazi kwamba rununu hizi sasa zimefikia tamati kwani “Hakuana marefu yasiyo na ncha” na zipo taarifa kuwa Samsung itaachana na utengenezaji wa Galaxy Note na Note 20 Ultra mwaka 2022.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania