Watumiaji wa WhatsApp wanazidi kuongezeka kila siku halikadhalika programu hiyo tumishi husika imekuwa ikiboresha mara nyingi tuu na utakubaliana nami kwamba huko nyuma haikuwezekana kusikiliza jumbe za sauti lakini leo suala hilo linawezekana.
Kwa miaka mingi sasa nimekuwa mtumiaji mzuri wa WhatsApp lakini pia mara moja moja nimekuwa nikituma jumbe za sauti kwenda kwa yule niliyemkusudia ingawa lazima nikiri kuwa kipengele hicho huwa kinanifanya niwafikirie rafiki zangu viziwi/wenye usikivu hafifu.
Kipengele cha uwezo wa kutuma na kupokea jumbe zilizo katika mfumo wa sauti kimekuwa kikiboreshwa na sasa kimezidi kupendezeshwa kwani taarifa zinasema wahusika wanakiboresha kipengele hicho kumuwezesha mtumiaji kuweza kusikiliza ujumbe husika katika kasi ya kawaida ama haraka iliyogawanyika mara mbili. Na kwa upande mwingine WhatsApp wameenda hatua kadhaa mbele na ni muhimu sote tukafahamu kwamba iwapo utausambaza ujumbe wa sauti kwenda kwa mtu/kikundi ndani ya WhatsApp basi kile kitufe cha kukuwezesha kuongeza/kupunguza kasi ya kusikiliza ujumbe huo HAKITAKUWEPO.

Kiukweli kipengele hiki kinanifanya nitabasamu hasa pale ambapo nawakumbukwa rafiki zangu wasioona na naamini hata wenyewe watakuwa wamefurahishwa na hili 😆 😆 😆 . Je, wewe msomaji wetu una lipi la kusema kuhusiana na habari hii?
Vyanzo: GSMArena, WaBetaInfo
2 Comments