Unakumbuka tuliandika habari kuhusu kutofanya vizuri kimauzo kwa Zantel na deni kubwa la takribani bilioni 159, (Soma hapa-> Zantel Yahaha kulipa Deni la Zaidi ya Bilioni 159!) mambo yamezidi kwenda mrama kufikia hatua ya wamiliki wakubwa wa kampuni hiyo kutaka kuuza umiliki wao!
Shirika la mawasiliano la Etisalat lenye umiliki wa asilimia 65% katika Zantel tayari limeanza kufikiria uwezekano wa kuuza umiliki wao ili kulipa deni hilo la dola za kimarekani milioni 96 ambalo Zantel inadaiwa na benki ya kijerumani ijulikanayo kama Deutsche Bank. Benki hiyo ishaanza kutishia kuchukua hatua za kisheria kama Zantel itaendelea kuchelewesha malipo hayo.
Shirika la Etisalat linamiliki asilimia 65% ya Zantel, huku asilimia 18 ikimilikiwa na serikali ya Zanzibar huku kampuni ya Meeco International ikiwa na asilimia 17. Etisalat inawabidi wafanye uamuzi huu kwani wao ndio waliodhamini mkopo huo wa Tsh bilioni 159.
Zantel pamoja na TTCL ndio wanaochukuliwa kuwa Watoaji wa Huduma ya Intaneti (ISP) wakubwa zaidi kwa Tanzania kutokana na uendeshaji wao wa mikongo ya intaneti itokayonje ya nchi. Wao ndio wauzao huduma hiyo kwa mashirika mengine ya simu, na taarifa za sehemu nyingi zinaonesha Zantel ndiyo namba moja katika Watoaji wa Huduma ya Intaneti (ISP) nchini.
Vodacom & Tigo ‘Wahaha’ Kupata Umiliki Huu!
Habari za chini ya kapeti zinaonesha makampuni haya mawili yote yashaonyesha nia za kutaka kununua umiliki huu. Kama Vodacom watanunua Zantel basi watazidi kujiweka juu zaidi wakati kama Tigo watafanikiwa basi nao wataongeza mabavu na kufanya ushindani kati yao na Vodacom na Airtel kuwa mkubwa zaidi. Na ZAIDI YA YOTE yeyote atayefanikiwa kuuchukua umiliki huu basi atajiweka vizuri zaidi katika huduma ya intaneti!
Je mambo yataishia vipi? Endelea kutembelea TeknoKona
No Comment! Be the first one.