fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Maujanja meseji Teknolojia whatsapp

WhatsApp: Mambo Ambayo Huenda Huyafahamu

WhatsApp: Mambo Ambayo Huenda Huyafahamu

Spread the love

Programu ya WhatsApp ni maarufu sana na kuna uwezekano mkubwa unaitumia ila unaitumia bila kutambua au kutumia hizi chaguzo chache za makundi, usiri na faragha, matangazo (Broadcast), kutuma ramani ya eneo uliopo na kuhamisha meseji kwenda kwenye simu mpya.

Kuhusu Makundi

Umeshawahi kujiuliza nini kinaweza kutokea iwapo ‘admin’ akaamua kufuta kundi na kujitoa ?

Makundi yanatengenezwa na kiogozi (‘admin’) na yeye ndiye mwenye uwezo wa kumuingiza mtu mpya kwenye kundi. Mtu yeyote anaweza kujitoa kwenye kikundi hilo na kulifuta kwenye simu yake bila kubadili chochote kwenye simu za wengine ila ‘admin’ akiamua kuingia mitini na kufuta kundi lake kwenye simu yake, WhatsApp haitafuta kundi hilo kwenye simu za wengine na badala yake itampa mtu mwingine uongozi na kundi litaendelea.

Badili unavyoshituliwa na simu kuhusu meseji za Makundi:

Kama unapenda kupata habari kutoka kwenye makundi ila unapata shida sana na milio ya simu kila sekunde, unaweza kufanya kati ya haya:

  1. Zima mlio, ‘Mute’ kwa muda flani: Masaa 8, wiki au hata ikiwezekana mwaka mzima kutegemea na muda unaotaka kuzima kundi hilo. Ingia kwenye kundi, bofya menu>Mute>chagua 8 Hours, 1 Week au 1 Year.

    androidpit-whatsapp-mute

    Menu> Settings> Zima Milio

  2. Potezea kabisa kundi. Kama hutaki kujua kinachoendelea kwenye kundi lolote mpaka uingie WhatsApp, toa kabisa notisi(‘notifications’) na milio ya kundi hilo kwa kuingia kwenye menu ya kundi, bofya mute na toa tiki iliyopo kwenye ‘Show notifications’. Hapo utakuwa umeziba kabisa macho na masikio kwa kundi hilo.
  3. Toa kabisa sauti kwa makundi yote. Hii ni kwa wale amabao hijalishi makundi yaliyopo wala mapya, hawataki bugudha aina yoyote. Ingia kwenye WhatsApp> menu> settings> notifications> Group notifiactaions> notification tone> silent.  Tiba tosha.

Hamisha Meseji kwenye simu mpya.

Ukibadilisha simu, unaweza kuhamisha meseji zako kutoka kwenye simu ya zamani na kuipeleka kwenye simu mpya kwa ku-‘back-up’ meseji zako na kulihamishia faili la WhatsApp kwenda kwenye simu mpya. Chukua tahadhari kwamba, namba yako inabidi ioane na namba ya WhatsApp unayoihamishia.

Fanya ‘Back-Up’ ya Meseji zako za WhatsApp

Jidhibiti kwa Usiri na Faragha

Faragha ni kitu muhimu na watu wanazidi kuamka kuhusu swala hilo. Kwenye WhatsApp, sasa unaweza kuficha ‘last seen’ ili  mtu asijue mara ya mwisho ulipotumia WhatsApp. Hata hivyo, kwa chaguzo hii ukiwa ‘online,’ mtu anaweza kujua na kama ukichagua chaguzo hii, hautaweza kuona ‘last seen’ ya mtu mwingine. Unaweza kuficha picha yako au status kwa watu wasiokujua na hata watu wote. Kufanya chaguzo ya faragha, ingia kwenye WhatsApp> settings> Account> Privacy na fanya chaguzo zinazokufaa.

Settings> Account> Rekebisha Faragha na Usiri (Privacy)

Tuma Matangazo

Unaweza kutuma matangazo kwa kutumia WhatsApp bila kutumia kundi.Kufanya hivi tumia menu> broadcast> chagua watu unaotaka kutangazia. Baada ya kuwachagua unaweza kutunza orodha hiyo ili kuitumia mara nyingine. Hii ni njia tofauti na makundi kwa sababu watu unakaowatumia wataweza kupata meseji kama vile umewatumia meseji ya kawaida na watakujibu kikawaida siyo kama kwenye makundi.

Broadcast Message

Tuma Matangazo kwa kubofya menu> ‘Broadcast message’

Tuma Ramani ya Eneo Uliopo.

Unaweza kutuma eneo ulipo kwa kutumia ramani ya Google maps, ili mtu apate maelekezo kwa ramani. Kufanya hivi tumia ‘attachments’ chagua location na tuma. Hapa utaweza kutuma yale maeneo yaliyo karibu yako tu.

screenshot_2013-04-13_1709-crop

Chagua ‘Location’ kutuma Eneo Uliopo

Tafuta Neno kwenye Mazungumzo

Kuna muda utataka kukumbuka ulichosema wakati fulani kwenye mazungumzo na mtu fulani. Ukibofya menu>search kwenye mazungumzo na huyo mtu utaweza kufanya hivyo. Baada ya hapo unaweza ku’copy’ na ku’paste’ popote unapotaka.

Tofautisha Milio ya Meseji ya kawaida na Meseji ya Makundi.

Ukiingia settings>Notifications, unaweza kubadilisha mlio upi utumike kwa meseji za kawaida chini ya mipangilio ya ‘Message Notifications.’ Hii itakusaidia sana pale unapotaka kujua ni aina gani ya meseji imeingia na kama unataka kuiona wakati unafanya mambo mengine ya msingi.

notifications

Tofautisha Milio ya Meseji ya kawaida na Meseji ya Makundi hapa

Soma Meseji bila kuifungua mwenyewe (automatiki).

Kwenye Mipangilio ya Notifications pia unaweza kufanya meseji itokee ili uisome wakati unatumia app nyingine kama vile kwenye Viber. Kwenye settings> notifications, Chagua mpangilio wa ‘Popup Notification’ na badili vile unavyotaka, skrini ikiwa ‘on’, ‘off’ au wakati wote ‘always show popup’.

AndroidPIT-WhatsApp-Popup-Notification

Soma Meseji bila kufungua kwa ‘Popup Notification’

Weka Shotkati za Mazungumzo na Mtu fulani kwenye ‘Home-screen’ yako.

Ukifungua simu, utakutana na kinachojulikana kama ‘home screen’, yani mwanzo. Ili kuongea na mtu fulani haraka, unaweza kushikilia jina la mtu huyo au kundi na kubofya ‘Add conversation shortcut’ kwenye WhatsApp au bofya menu>more>Add shortcut ukiwa kwenye mazungumzo tayari. Ukifanikiwa, unaweza kurudi mwanzo na kuona picha ya mtu au kundi ambapo utatumia kuongea nae kirahisi.

create-shortcuts-to-whatsapp-conversation

Shotkati za Mazungumzo

Je, unajua kwamba WhatsApp inatumika na zaidi ya watu milioni mia sita? Kama unapenda kujua zaidi kuhusu WhatsApp au unapata shida na haya maujanja yaliyoorodheshwa hapa, unaweza kutupata teknokona kwa kubofya kati hizi – barua pepe, facebook na twitter.

 

Picha Na:

deccanchronicle.com, androidpit.com, tothemobile.com, android.stackexchange.com, nerdsmagazine.com, theandroidportal.com, truetechkings.blogspot.com,  na androidpasion.com.

SOMA PIA  Samsung wabeba prosesa zote za kisasa za Snapdragon 835 kwa ajili ya Galaxy S8 - wengine wazikosa
ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania