Checky inajibu swali dogo! Natumia simu yangu mara ngapi kwa siku? Jibu ni mara nyingi (ha!). Hii App inakuambia ni mara ngapi umetumia simu kwa siku na pia inatoa ramani ya sehemu ulizotumia simu hiyo. App hii inasaidia sana kama mtu simu huwa inakupotezea mda sana na unapenda punguza matumizi.
Haipingiki kuwa kuna mambo mabaya katika maisha yetu yanayosababishwa na teknolojia hasa kwa teknolojia ile iliyopo upande wetu kila saa: Simu-janja (SmartPhone) zetu. Ni karne ya 21, huelewi kitu? unaangalia simu yako, unataka jua kitu unaona aibu kuuliza? unaangalia simu yako. Upo kwenye foleni? Basi unatazama simu yako. Mtu kakuangalia jicho baya? Haraka! Unaamia kwenye simu yako kutwiti au kuandika Facebook kuhusu hilo jambo.
“Kama Watu Wengi, Naipenda Sana Simu Yangu” alisema mwanzilishi wa Calm, Alex Tew
Labda nikuulize swali hivi ni mara ngapi umetoa simu mfukoni kwa lengo la kuangalia saa lakini ukajishangaa unafanya mambo mengine? Ndio kabisa hii sio habari mpya kwetu, tunajijua kabisa hatujiskii kawaidi bila kuingiza mikoni kwenye mifuko na vipochi vyetu ili kutoa na kuangalia simu zetu mara kwa mara na hii imekua ni tabia.
Checky imetengenezwa na Calm lakini sio bidhaa ambayo walitumia muda kuikuza. Checky ni app rahisi sana na madhumuni yake mengine ni kuleta kiki kwa kampuni, ambayo imedhamiria kuingiza hela kupita App baadae.
Baada ya kujua taarifa jua ya matumizi ya simu yako unaweza amua ku ‘share’ katika mitandao ya kijamii. Kwa wale wenzangu wenye tabia za kusahau simu zao, App hii haitakua rafiki mzuri kwao. Hata hivyo simu zinasababisha ajali, kutumia simu kidogo na kwa mambo muhimu ndio mpango mzima!
Kushusha CHECKY bofya hapa iOs | Android
Je App hii unaipokea vipi? unaona kama inambana mwenye simu? changia mada yako hapa chini au kupitia akaunti zetu za Twitter na Facebook
No Comment! Be the first one.