fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Teknolojia

App Ya Uber Inabadilisha Maisha Ya Wanawake Wa Saudi Arabia!

App Ya Uber Inabadilisha Maisha Ya Wanawake Wa Saudi Arabia!

Spread the love

Katika nchi ambayo huruhusiwi kuendesha gari, utafika vipi au utazururaje mjini?. Hii ni kwa wanawake wa saudi arabia, Nchi ambayo ina sera maalamu isiyoruhusu wanawake kuendesha magari. Kwa wanawake wengi wa Saudi Arabia App ya Uber ndio kimbilio lao.

Ukiachana na mapendekezo yaliyotolewa na Baraza linalojulikana kama Shura, Kamati ya ushauri ya saudi (Ambayo ki ukweli inakuja na vizuizi vya aina yake). Wanawake bado wanakatazwa kuendesha katika nchi hiyo tena wanakatazwa ikiwa inaogopeka wanaweza kuvunja sheria kama vile kuvua jilbaab,hijab au hata sheria nyingine ya kidini inayohusika na kufunika uso kwa mwanamke ambayo inamfanya awe anaelekeza vizuri macho yake kwenye barabara.

Wanawake Wa Saudi Arabia Wao ni Siti Ya Nyuma Tuu!

Wanawake Wa Saudi Arabia, Wao Hawaijui Siti Ya Dereva !

Ingawa hakuna sheria ya kawaida (General Law) ambayo inamkataza  mwanamke kuendesha gari. Lakini pia leseni si ndio kila kitu, yaani ndio itakayo kuruhusu kuendesha gari? Cha kushangaza ni kwamba Saudi Arabia hawatoi leseni za udereva kwa wanawake. Ikitokea amekamatwa anaendesha gari adhabu na sheria kali zitachukuliwa.

Kutokana na adhaa hiyo, wanawake wengi wanalazimika kutumia huduma za magari kama vile Taxi kufika katika miji mikubwa kama vile Riyadh, Dammam, na Jeddah.

Mwanamke Wa Saudi Arabia Akificha Uso Wake Huku Akiwa Kakaa Siti Ya Dereva Akionyesha Funguo

Mwanamke Wa Saudi Arabia Akificha Uso Wake Huku Akiwa Kakaa Katika Siti Ya Dereva Akionyesha Funguo

Ingiwa wanawake wa saudi wanachangia asilimia 13 tuu kama nguvu kazi katika nchi hiyo (Saudi Arabia). Inasemekana (Haina usahihi kwa asilimia 100)  kuwa asilimia yoyote kati ya 70 na 90 watumiaji wa Uber nchini saudi arabia ni wanawake. Kama inavyojulikana Uber ni App ambayo inatumika kwa madereva kuwaonyesha ruti tofaui tofauti katika sehemu husika.

SOMA PIA  Tanzania kushuhudia tukio la kupatwa kwa mwezi leo.

Nchini Saudi Arabia asilimia 60 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni jinsia ya kike kulingana na takwimu zilizilizotolewa na  Fast Company, zinaonyesha kuwa wanawake hasa kwa sasa wanatakiwa watoke na wazurure na sio zile sehemu ambayo inawabidi wawe tuu bali hati zile wanazohitaji kuwepo

Moja Kati Ya Picha ZInazotumiaka Mitandao Na Hata Katika Maandamano Juu Ya Haki Za Wanawake Juu Ya Kuendesha Magari

Moja Kati Ya Picha ZInazotumiaka Mitandaoni Na Hata Katika Maandamano Katika Haki Za Wanawake Juu Ya Kuendesha Magari

App Ya Uber Ilianza Patikana Kwa Wananchi Wa Saudi Arabia May 2014. Tokea hapo imekuwa ni msaada mkubwa kwa wanawake ambao sera ya kutoendesha gari inawabana

Katika mahojinao yaliyofanyika baina ya  Fast Company na Meneja mkuu wa Uber bw. Majed Abukhater alieleza kwa kina juu ya tofauti zipi aliziona tangia App ya Uber inaze kufanya kazi nchini Saudi Arabia na mabadiliko hayo haswa yamefanywa na wanawake.

SOMA PIA  Google kufanya masasisho ya kwenye apps zake kuongeza usalama

”Muda mwingine makampuni ya usafiri  yalikuwa yanakata tiketi kwa wananchi wa nchi hiyo na kujaza viombo vyao vya usafiri lakini wananchi wengine wakikosa usafiri kutokana na makampuni hayo kusaza. Wanamke kwa upande mmoja au mwingine wangepata shida kuenda sehemu fulani za jijini hapo” alisema Abukhater ”Kwa kuwa tumeongeza teknolojia hii nchini humu sasa mwanamke hatahitaji kupigia simu kwa makampuni  10 au 20 ili kujaribu kupata dereva, wanaweza tuu wakafungua App. Hivyo ndio maana tumeona ongezeko kubwa (ukuaji) mpaka sasa”

 Chanzo: Fast Company 

Kwa nchi ambayo mtu huwezi (huruhusiwi) kuendesha gari kabisa, App kama hii ambayo itakuonyesha njia na ruti mbalimbali inaweza ikawa ndio kimbilio lako kubwa. Uber inaonyesha ukombozi mkubwa juu ya jambo hili. Tuambie habari hii wewe umeipokeaje? achana na Tanzania unapoweza  endesha (hata kwa kinyemela kama huna leseni halali hah!) sema Saudi Arabia ukionekana ni mwanamke tuu na unaendesha, hakuna maelezo!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania