Maendeleo katika ufuati wa umeme utokanao na Jotoardhi yanakuja. Kampuni kubwa ya vifaa vya umeme hasa hasa elektroniki na mashine mbalimbali ya Toshiba ya nchini Japani imeripotiwa kuingia mkataba na shirika la maendeleo ya nishati ya jotoardhi la TGDC la Tanzania.
Shirika la TGDC, yaani Tanzania Geothermal Development Company Limited ni shirika lililo chini ya TANESCO likiwa na jukumu kuu la kupromoti maendeleo ya sekta ya ufuaji umeme kwa kutumia vyanzo vya nishati ya jotoardhi (kimombo -Geothermal).
Tanzania inashika nafasi ya tatu Afrika kwa kuwa na maeneo mingi yenye miamba ya yenye joto kali yenye uwezo wa kutumika kufua nishati ya jotoardhi lakini imekuwa nyuma katika kuvitumia. Utumiaji mkubwa wake mkubwa duniani ni katika ufuaji wa nishati ya Umeme, TGDC imepewa mamlaka spesheli Tanzania katika kuendeleza maendeleo ya sekta hii.
‘Geothermal energy’ inatumikaje kuzalisha umeme?
Kwa kutumia njia njia spesheli za kusafirisha joto kali lililopo kwenye miamba ya moto, joto hilo kupitia mvuke mkali hutumika kuendesha mitambo inayo zalisha umeme.
Toshiba ina miaka mingi ya ujuzi katika eneo la ufuaji wa umeme kwa kutumia jotoardhi. Duniani kote imesambaza majenereta zaidi ya 52 ya kuzalisha umeme kwa kutumia jotoardhi. Kwa barani Afrika wanahusika na mitambo ya uzalishaji wa umeme wa mfumo huu nchini Kenya.
Kwa Tanzania watasaidiana na TGDC katika kutengeneza utaratibu, kufanya utafiti, kuwapa watanzania ujuzi katika teknolojia hiyo na kusimamia uwekaji wa mitambo ya uzalishaji umeme kwa chanzo hiki.
Pongezi wa TGDC kwa hatua hiyo.
Vyanzo: Renewableenergyworld.com, esi-africa.com
No Comment! Be the first one.