fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Kompyuta

Microsoft Office 2016, Office 365 : Andika na Kusoma Mafaili Kwa Ushirikiano na Wengine

Microsoft Office 2016, Office 365 : Andika na Kusoma Mafaili Kwa Ushirikiano na Wengine

Spread the love

Microsoft wanazidi kusambaza apps za kisasa kabisa katika kifurushi chao cha huduma ya Office 365. Kwa watumiaji wa huduma ya Microsoft Office 365 sasa watapata pia toleo jipya kabisa la Microsoft Office 2016.

Kuna tofauti gani kati ya Office 365 na Office 2016 (au programu nyingine yeyote ya Office)?

Huduma ya Office 365 ni kivurushi cha huduma mbalimbali za Office ambacho ukilipia – kwa mwezi, au mwaka basi unapata ndani huduma mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutumia toleo jipya kabisa la programu ya Microsoft Office.office365

Wakati unaweza kununua diski ya Microsoft Office kawaida ila huduma ya Office 365 inapatikana kupitia mtandao, namaanisha kujiunga itabidi ulipie mtandaoni na kisha utaweza kushusha na kupakua (download na install) programi/apps za Microsoft Office kwenye kompyuta, tableti au simu yako. Mfumo wa malipo unakuwa wa kwa mwezi au kwa mwaka, uinunue moja kwa moja.

Huduma zinazotengeneza kifurushi cha Microsoft Office 365

 • Unapata huduma ya uhifadhi mafaili kupitia mtandao – yaani Cloud, kupitia OneDrive
 • Unapata uwezo wa kuweka na kutumia huduma za Office kwenye vifaa vingi bila malipo ya ziada. Kwa mfano kama unalipia kifurushi cha Office 365 cha Binafsi (Personal) basi utaweza kupakua na kutumia apps za Office 2016 kama vile Excel, Word na PowerPoint kwenye kompyuta 1 (Windows au Mac), kwenye tableti 1 (iPad au ya Android) na pia kwenye simu moja.
 • Pia unapata hadi dakika za maongezi kupitia huduma ya Skype (dakika 60 za bure kila mwezi za kupiga simu kokote duniani)
 • Utaendelea kupata masasisho (updates) ya huduma za Office bure kabisa muda wote wa malipo ya kifurushi chako.

*Kwa sasa kifurushi cha Microsoft Office 365 cha matumizi binafsi (Personal) kinauzwa kwa takribani Tsh 150,000/= (dola $69.99) kwa mwaka au Tsh 16,000/= (Dola $6.99) kwa mwezi.

 • Kupitia huduma ya OneDrive mtumiaji ataweza kuendelea alipoachia kufanyia kazi document yake kwenye kifaa kingine. Mfano unaweza ukaandika nusu ukiwa kwenye kompyuta na utaweza fungua na kuendelea kuifanyia kazi document hiyo kwenye simu au tableti yako.
SOMA PIA  TikTok inajaribu kitufe cha 'repost' ili kushambaza klipu na marafiki

Microsoft Office 2016 ni toleo jipya kabisa la huduma ya Microsoft Office na linakuja na mambo mbalimbali ya kuvutia kama ifuatavyo;

 • Kupitia huduma ya Office 365 watumiaji kadhaa wanaweza wakashiriki kwa wakati mmoja kuandika na kurekebisha document moja.

  Watu wengi wanaweza shiriki kwa wakati mmoja kuandika na kufanya marekebisho ya document moja. Kila kitu kinachofanyika kitakuwa 'live' kwa wote

  Watu wengi wanaweza shiriki kwa wakati mmoja kuandika na kufanya marekebisho ya document moja. Kila kitu kinachofanyika kitakuwa ‘live’ kwa wote

 • Ingawa Office 2016 inakuja na apps mbalimbali zilizoboreshwa kama vile Word, PowerPoint, Excel, Outlook, OneNote, Project, Visio na Access – kama umejiunga na kifurushi cha Office 365 utaweza kupata masasisho (updates) kwa wakati kabisa. Kuhakikisha mara zote unatoleo jipya zaidi la apps hizo.
 • Skype imeboreshwa zaidi kutumika sambamba na apps za Microsoft Office

Ata kama watumiaji watakuwa mbali wataweza kuzungumza, kuchati na kutumiana picha za wanachokiona kwenye kompyuta zao bila kuondoka kwenye programu hizo za Office. Yaani Skype inakuwa kama sehemu moja ndani ya programu hizo za Office.

Chati za Excel zimeboreshwa zaidi

Chati za Excel zimeboreshwa zaidi

Mambo mengine yaliyoboreshwa katika Office 2016 ni pamoja na;

Outlook; Programu hii spesheli ya kusoma, kuandika na kutuma barua pepe imeboreshwa na imekuwa janja (smart) zaidi. Sasa itaweza tambua ni barua pepe gani ni muhimu zaidi kuwa juu na zipi si za muhimu sana kupewa uzito.

‘Tell Me’ na ‘Smart Lookup’, hizi ni maboresho katika kukusaidia kujua kitu chochote cha kwenye programu ya windows kinapatikana wapi. Yaani kama kuna kitu unajifunza jinsi ya kukifanya basi Smart Lookup itakusaidia kuonesha kwa urahisi, na hii itahusisha ata kukutafutia vyanzo vya mtandaoni.

Excel; Kuna maboresho ya mfumo mzima wa chati za kuonesha data kwenye Excel. Sasa zitakuwa nzuri na za kuvutia zaidi.

‘RecentDocuments’; Hii ni sehemu ya kuangalia document uliyofungua hivi karibuni, kupitia muunganisho na programu ya One Drive chini ya huduma ya Microsoft Office 365 basi utaweza kufungua ata document uliyoifungua hivi karibuni kwenye kompyuta au kifaa chako kingine na kuendelea mara moja pale ulipoishia.
Apps (programu) za Microsoft Office 2016 zinapatikana tayari moja kwa moja kupitia mtandao wao na kwa wale ambao tayari ni wateja wa vifurushi vya Office 365 basi wataweza kushusha na kupakua apps za Office 2016. Kwa nchi kama zetu, zinazoendelea, ambazo bado suala la intaneti ya kasi kwa wengi bado ni shida Microsoft wamesema wataendelea kuuza Office kwa mfumo wa DVD pia, hivyo vuta subira na hivi karibuni utaona DVD za Office 2016 zikianza kupatikana.

Microsoft wanashauri, Office 2016 inaendana vizuri zaidi na toleo jipya la Windows. Yaani Windows 10

Microsoft wanashauri, Office 2016 inaendana vizuri zaidi na toleo jipya la Windows. Yaani Windows 10

Je una mtazamo gani juu ya teknolojia ya Office 365? Sisi tunaona suala la bei linaweza likawa kikwazo kwa wengi, ila ukithaminisha unachopata na kama ni mtu wa kazi sana basi ni dili poa. Unatumia toleo gani la Microsoft Office kwa sasa?

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

 1. […] Soma kuhusu Office 365 na Office 2016 – Microsoft Office 2016, Office 365 : Andika na Kusoma Mafaili Kwa Ushirikiano na Wengine […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania