Wakati taarifa zikisema ya kwamba Xbox One itaweza kucheza magemu ya Xbox 360, watu wengi wamegeuzia macho yao kwa Sony kuona watajibu vipi mapigo hayo na PlayStation 4 (PS4).
Wakubwa wa kampuni ya Sony wameeleza mara kwa mara kwamba hawana mpango wa kufanya magemu ya PS3 kuchezeka kwenyee PS4. Kampuni hiyo sasa inataka kufanya uwezekano wa kucheza magemu ya zamani sana kwenye konsoli yake mpya.
Habari hizi zinakuja kufuatana na taarifa kwamba magemu kadhaa ya PS2 yalioambatanishwa na Star Wars Battlefront PlayStation 4 yanaweza kuchezeka kwa teknolojia maalumu kwenye PS4. Hii ina maana kwamba upo uwezekano wa kuleta magemu mengine ya PS2 kwenye konsoli ya PS4, na pia msimamo wa kampuni ya Sony walipohojiwa na EW.
Jambo la kuwezesha kuchezeka kwa magemu ya zamani si kitu kigeni. Ikumbukwe kwamba Sony walifanya hivyo kwa PS3 waliporuhusu magemu kadhaa yaliopendwa na wengi katika PS2 na PlayStation ya kwanza kuchezeka.
Hizi huenda zikawa habari nzuri kwa watu wanaomiliki CD za zamani au nakala za magemu ya zamani yasiopatikana kwenye konsoli mpya au ambazo zimeachwa kutengenezwa tena na zinapendwa na wengi.
Chanzo: ew.com
No Comment! Be the first one.