fbpx
Android, apps, Google, Teknolojia

Watu 12 kuweza kujumuika kwenye Google Duo

watu-12-kuweza-kujumuika-kwenye-google-duo
Sambaza

Inawezekana kabisa ukawa miongoni mwa watu ambao hawaamini katika mawasiliano ya kupitia picha jongefu (mnato/video) lakini wakati huu ambao dunia inapambana na virusi vya COVID-19; teknolojia hiyo ndio mkombozi wa wengi ukiacha Skype, WhatsApp na hata kwenye Google Duo.

Google ni moja ya makampuni ambayo huwa hayaoni hiyana kuachana na kitu kama wanaona hakina watumiaji wengi/umaarufu wake umeshuka. Mwezi Agosti 2016 kampuni hiyo iliruhusu programu tumishi iitwayo Google Duo kuweza kupatikana kwenye App store au Playstore kwa simu janja zenye Android 4.1 kuendelea ama iOS 9 kwenda mbele. Na tangu wakati huo imekuwa hewani. Kufahamu zaidi kuhusu Google Duo BOFYA HAPA.

INAYOHUSIANA  Huduma ya Usafiri wa Uber Kuja Tanzania, Uganda na Ghana

Teknolojia ya kutumia picha mnato kufanya mawasiliano wakati kila mtu akiwa kwake kwa usaidizi wa intaneti imekuwa ni jibu sahihi katika kuhakikisha watu hawakusanyiki kujadili mambo ana kwa ana ili kuepusha kuenea kwa virusi vya Corona vinavyosababisha homa ya mapafu. Google wameona inafaa kuiongozea uwezo programu tumishi husika kutoka watu wanane (8) wanaoweza kuwasiliana kwa wakati mmoja hadi kumi na wawili (12).

INAYOHUSIANA  SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400
kwenye Google Duo
Google Duo: Watu wasiozidi kumi na wawili hivi sasa wanaweza kuwasiliana kwa wakati mmoja.

Ndio, hivyo ambavyo ambavyo umuhimu wa kutumia teknolojia ya kuonana kupitia bidhaa za kielekroniki ukiongezeka wakati huu ambapo serikali za nchi nyingi zimeamrisha watu wake wakae majumbani.

Vyanz0: 9To5Google, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Uwezo wa watu wanne au zaidi kuweza kuwasiliana kupitia WhatsApp
    April 19, 2020 at 9:39 am

    […] Watu 12 kuweza kujumuika kwenye Google Duo […]