fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Teknolojia Twitter

Twitter inaboresha namna ambavyo watu wanaweza kuonyesha hisia zao

Twitter inaboresha namna ambavyo watu wanaweza kuonyesha hisia zao

Spread the love

Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii ambao umejikita zaidi kuhabarisha, kukutanisha na watu lakini katika mtindo wa kipekee kabisa kuanzia idaidi ya maneno kwa chapisho, muonekano wake na sasa inaboreshwa kutanua wigo wa watumiaji kuonyesha hisia zao.

Unachapisha kitu kwenye Twitter watu  mbalimbali wanaweza kupendezwa na kile ambacho umekiweka hivyo basi idadi ya wanaume kwa wanawake waliovutiwa wataonekana tuu.

SOMA PIA  Apps Za Mahusiano Zahusishwa na Ongezeko la Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono

Katika kile ambacho kinapikwa kwenye Twitter wahusika wanaweka mambo sawa na kuongeza namna ambavyo watumiaji wa Twitter wanaweza kuonyesha hisia zao kwenye chapisho ambalo mtu ameliweka. Katika siku za usoni mtu ataweza kuonyesha ishara ya kufurahishwa kwa kucheka, huzuni, kuguna.

SOMA PIA  Huawei yashauriwa kuweka nguvu kwenye utengenezaji wa programu wezeshi

Huu ni kama mwendelezo wa kuboresho vitu vya mtindo kwani mtandao huo wa kijamii ulishaongeza mtindo huo wa kuonyesha hisia kwenye uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maandishi ambapo mtumiaji anaweza kuuweka kikatuni fulani kama ishara ya kufurahi, kupenda, kulia, kukasirika, n.k.

kuonyesha hisia zao

Alama mbalimbali za kuonyesha hisia zako zasongezwa kwenye uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maandishi.

Maboresho haya yatakuwa sehemu ileile kama iliyo kwenye Facebook kwa maana ya kwamba kwenye kitufe cha “Like” (penda) kisha kuchagua kile ambacho ataona kinafaa kulingana na chapisho husika.

SOMA PIA  Simu za Google Pixel zapata muonekano wa giza

Unawaza kuhusu lini maboresho hayo yataanza kupatikana? Tutegemee kuona kitu hicho ndani ya wiki chache zijazo. Kuna mengi ambayo Twitter imeboresha na vingine kuwa vitu vipya kabisa. Je, unaizungumziaje Twitter ya sasa?

Vyanzo: The Verge, DNA India

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania