Kampuni ya Lexus imekamilisha kutengeneza skateboard iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa michezo ya kuteleza, skateboard hiyo ambayo inaelea hewani na iliyopewa jina la slide imekuwa gumzo kubwa kwa wapenzi wa wa kuteleza.
Ubao huo wakutelezea unafanya kazi kutumia teknolojia inayotegemea nguvu ya usumaku katika joto la chini sana, sakafu inayotumika ni sakafu yenye nguvu za usumaku na ubao huo wa kuteleza umetengenezwa na semiconductor na unapoozwa kufikia katika joto la (-197c) hii inawezekana kwa msaada wa nitrojeni iliyo katika hali ya kimiminika. Muunganiko wa sakafu (yenye usumaku) na semiconductor hizo katika nyuzi joto za centigredi -197 ndio hufanya ubao kuelea.
Teknolojia hii inaitwa magnetic levitation (maglev) na ilitumiwa kwa mara ya kwanza kutengeneza ubao wa kutelezea ulioitwa Hendo huu ulikuwa unachajiwa kwa saa moja ama masaa mawili kwaajiri ya kutumika dakika 15 pia ulikuwa unatumia bateries , pia teknolojia hii imetumika kutengeneza treni ya mwendo kasi ya huko shanghai ambayo inaweza kwenda katika mwendo wa km 600 katika saa moja.
Ubao huu ambao unauzito wa kilo 11.5 na umetengenezwa kwa kutumia aina ya matete kwa kiasi kukubwa, unaelea katika kima cha sentimita mbili na nusu. Ulitengenezwa kufuatisha filamu ya mwaka 1989 ya Back to the future II ambayo ndiyo iliyoiongelea hii teknolojia ya ubao kuelea hewani kama hivi, kipindi hicho hii ilikua ni ndoto tuu.
Hata hivyo ni mapema sana kuzitegemea kuuona huu ubao mitaani maana ili ubao huu ufanye kazi unahitaji sakafu maalumu yenye usumaku. Ila katika miaka ya mbeleni labda viwanja hivyo vitatengenezwa na hivyo skateboard hizi kuweza kutumika. Watafiti wengi wameona teknlojia hii inaweza ikaja kutumika kutengeneza magari yanayoelea hewani pia. Tuambie maoni yako.
No Comment! Be the first one.