Katika ulimwengu wa sasa teknolojia ya 5G inaendelea kushika kasi kwani makampuni mengi yamekuwa yakiwekeza kwa kiasi kikubwa na kuja na vifaa vya kidijiti ambayo vina uwezo wa kuendana na kasi ya teknolojia husika.
Honor ambayo hapo awali ilikuwa chini ya mwamvuli wa Huawei lakini ikaamua kusimama yenyewe na kutoa bidhaa zake hivi karibuni wamezindua simu janja Honor X8 5G ambayo imejaa vitu vingi ninavyovutia wateja katika ulimwengu huu wa sasa. Mwezi Machi mwaka huu Honor X8 ilizinduliwa ambayo kimsingi haina tofauti kubwa na toleo lililotoka hivi karibuni. Honor X8 5G ina sifa zifuatazo:-
Muonekano|Kipuri mama
Hapa tunakutana na simu janja yenyr kioo cha urefu wa inchi 6.5 IPS LCD (720*1600px) ambapo kwa uso wa mbele kamera mahususi kwa ajili ya kujipiga picha imenakshiwa kwa mtindo wa kuingia ndani kidogo mithili ya bonde la ufa. Kwa upande wa kipuri mama simu hii imewekwa Snapdragon 480+ SoC.

Menori|Betri
Kwenye kipengele hiki tunakutana na RAM ya GB 6 kwa 128GB diski uhifadhi pekee. Upande wa betri simu hii ina 5000mAh, teknolojia ya kuchaji haraka kwa 22.5W.
Kamera|Mengineyo
Simu hii ina jumla ya kamera 3+taa ya kuongeza mwangaza. Kamera kuu ina 48MP na nyingine mbili zina MP 2 kila moja. Inapatikana kwenye rangi ni Nyeusi na Bluu pekee. Ina Bluetooth, teknolojia ya kutumia alama ya kidole.

Kiuhalisia Honor X8 5G imepunguzwa vitu vingi ukilinganisha na toleo la awali; kuanzia kwenye ubora wa kamera, kipuri mama. Bei yake bado haijawekwa wazi na kama ni uamuzi wa kuinunua utategemeana na wewe unapenda simu janja ya namna gani.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.