fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple apps iOS 15 Teknolojia

Ujio wa iOS 15 ni Septemba 20

Ujio wa iOS 15 ni Septemba 20

Spread the love

Applewameendeleza desturi yao ya kutaja tarehe ya uzinduzi wa vitu vyao vingine wakati wa kutambulisha iPhone 13 na ndugu zake. Sasa tarehe ya ujio wa iOS 15 ni Septemba 20.

Apple ambao walizindua toleo la sasa la iPhone hawakusahau pia kueleza ujio wa bidhaa zao nyingine na hapa nikizilenga zaidi programu endeshi mbalimbali ambazo zinatumika kwenye iPad halikadhalika saa janja. Wakati iOS 15 inatoka mnamo Septemba 20 ya mwaka huu halikadhalika iPadOS 15 na watchOS 8 zitatoka.

Yaliyomo kwenye programu endeshi iOS 15/iPadOS 15

Programu hizo endeshi ambazo zinatoka kwenye familia moja lakini kutumika kwenye vifaa viwili tofauti zinaezwa kuwa na mengi lakini ambayo yanaonekana kwa urahisi ni:

Uwezo wa kuchuja taarifa fupi. Katika toleo hilo inaelezwa mtumiaji kuwa na uwezo wa kuzuia kupokea taarifa fupi kutoka kwenye programu tumishi/mtu fulani. Vilevile, uwezo wa kubadilisha muda (saa), kupanga taarifa za vile ambavyo umepanga kuvifanya kwa siku husika.

Ujio wa iOS 15

Kwenye iOS 15 inawezekana kusogeza karibu kwa yale ambayo yapo kwenye kalenda pamoja na maelezo kuhusu tukio husika.

FaceTime iliyoboreshwa. FaceTime ya kwenye iOS 15 inaelezwa kumuwezesha mtumiaji kuzuia kabisa zile sauti ambazo zinaleta bugdha wakati unapowasiliana na mtu kwa njia ya picha jongefu.

SOMA PIA  Infinix Note 7: Simu yenye muonekano na ubora mzuri. #Uchambuzi #Bei

Uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno. Inaelezwa kuwa kwenye toleo hilo linaliofuata la programu endeshi mtu atakuwa na uwezo wa kutafuta picha, picha mnato, nyaraka, n.k ambazo amezituma kwenda kwa mtu mwingine.

Uwezo wa kubadili ujumbe wa maadishi. Kwa kutumia kamera itawezekana kubadili ujumbe ulio katika mfumo wamaandishi ambapo mtu anaeza akahariri na hata kusambaza kwa wengine. Kipengele hicho ambacho pia kinafanana na Google Lens kwa upande wa Android pia inawezekana kutambua mnyama, mmea, picha iliyochorwa kwa kutumia kamera.

Vitu vingine ni kipengele cha SmartPlay, mbinu ya kumlinda mtoto kwa njia ya kidijitali ambapo mfumo utakuwa unapitia picha kuangalia kama zipo zile ambazo zinamdhalilisha mtoto ingawa hii inaelezwa kuwa haitaingiliana na sera inayozuia kuingilia faragha. iPadOS 15 inaelezwa kuboresha uwezo wa kufanya kitu zaidi ya kimoja katika mtindo ambao kioo kinakuwa kimegawanyika.

Ujio wa iOS 15

Muonekano wa mafaili yaliyofunguliwa kwenye iPad Pro inayotumia iPadOS 15.

Haya sasa tumeweza kufahamu machache kuhusu toleo la programu enedhi linalokuja zikihusisha iPhone, iPad. Mengi zaidi tutayaleta hapa mara zitakapokuwa zimeshatoka.

Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania