fbpx

Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Jumapili ya Julai 8, 2018 saa 11:15 jioni ndege mpya ya Serikali aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kwa mara ya kwanza ilitua katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Ndege hiyo ni ya nne kuwasili kati ya saba zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) kuimarisha huduma zake.

Rais John Magufuli, makamu wa rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ni miongoni mwa viongozi  walioshiriki katika mapokezi ya ndege hiyo.

INAYOHUSIANA  Elon Musk: Nenda kokote duniani ndani ya lisaa, usafiri kwenda Mirihi (Mars) unakuja

Je, unaijua ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner? Kupitia hapa teknokona tutakujuza wasifu wa ndege hiyo inayotarajia kuanza huduma zake hivi karibuni.

Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ya ukubwa wa wastani, yenye injini mbili inayotengenezwa na kampuni ya Boeing ya Marekani. Matumizi yake ya mafuta ni wa asilimia 20 chini cha ndege ya ukubwa sawa na huo na ndiyo ndege ya Boeing inayotumia kiwango cha chini zaidi cha mafuta.

INAYOHUSIANA  Soma Taarifa Kwa Umma Kutoka TCRA Juu ya Faini Kwa Makampuni ya Simu

Injini zake zimejengwa kwa njia maalum ili kupunguza sauti ndani na pia nje ya ndege kwa hadi asilimia 60. Madirisha yake ni makubwa kuliko ya ndege zingine za ukubwa kama huo kwa asilimia 30.

Kinyume na mfumo unatumiwa kawaida wa kufungua kuongeza au kupunguza mwangaza wa dirisha kwenye ndege, kwa ndege hii nii kiponyezo hutumika kwa kutumia teknolojia ya kabadilisha rangi ya kioo kukiwezesha kudhibiti mwangaza unaoingia.

 Boeing 787-8 Dreamliner

Ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyoletwa kuimaeisha usafiri wa anga nchini Tanzania.

Ina uwezo wa kubeba hadi abiria 262 ikiwa pia na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 13,621 bila kusimama. Boeing 787-8 ilijengwa kuchukua mahala pa ndege aina za 67-200ER na 300ER ambazo pia ni ndege zinazomilikiwa na Tanzania.

INAYOHUSIANA  TCRA: Utumiaji Wa Simu Feki Umeshuka!

Tanzania imezidi kujidhatiti katika kuongeza ufanisi na ushindani katika huduma ya usafiri wa anga ambayo kwa miaka mingi ilikuwa imeyumba  (haifanyi vizuri).

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.