Wengi wanasubiria kwa hamu kufahamu Samsung wataleta nini cha utofauti katika toleo lao lijalo la simu za familia ya ‘Galaxy S’. Yaani Samsung Galaxy S6.
Hadi sasa tayari mambo kadhaa yameanza kujulikana, (kumbuka kuna ambayo yanaweza kuwa tofauti) nayo ni haya;
- Kioo kitakuwa kimefunika hadi eneo la kona za juu na chini, kimombo wanaita ‘Curved’.
- Inawezekana mfuniko wake wa nyuma ukawa wa madini ya chuma na si plastic kama matoleo yaliyopita.
- Kuna uwezekano kukawa na matoleo mawili ya Galaxy S6. Moja ya muonekano wa kawaida na nyingine yenye umbo la mpindo (curved).
- Inasemekana kwenye Galaxy S6 Smasung wamepunguza ujazo wa Apps nyingi zisizokuwa za ulazima kutoka kwao kitu ambacho kilikuwa kinalalamikiwa sana. Hivyo tegemea kutoona apps kama vile ChatOn, Samsung Hub, My Galaxy, n.k
SIFA ZINGINEZO
- Kioo cha inchi 5.2 au 5.3
- Kamera ya nyuma – Mega Pixel 20! (Kwa kiwango hichi picha zitakuwa za kiwango kikubwa sana.
- Betri ya 2600mAh (Si kiwango kikubwa)
- Kuna vyanzoi vingi vinasema itakuwa na RAM ya GB 4
- Kutakuwa na toleo lenye diski uhifadhi wa GB 32,64 na 128
- Kuna uwezekano mkubwa ikaja na toleo la Android Lollipop (Android 5)
Utambulisho rasmi kutoka Samsung wa simu hii unategemea kufanyika mwezi ujao (Wa tatu), endelea kusoma TeknoKona.Com na tutakuelezea mambo yatakavyokuwa!
No Comment! Be the first one.