TCRA imetoa taarifa kwa umma kuhusu suala la makampuni ya simu kupandisha bei ya vifurushi hasahasa kwenye suala la intaneti. Ila katika hali isiyokuwa inategemewa haijaweka bayana kama imechukua hatua yeyote dhidi ya makampuni hayo kutokana na kile ambacho wengi na hii ikiwa ni pamoja na Mheshimiwa January Makamba, Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuona kuna hatua kadhaa kama vile kutangaza bei hizo kabla ya mabadiliko kutofuatwa.
Kwenye taarifa hiyo kwa umma imeelezea hali ya sekta ya mawasiliano na hali ya gharama zake.
{Bofya kusoma – Mhe. J. Makamba ‘Tumewaandikia TCRA Wachukue Hatua …..’}
Katika taarifa iliyotolewa na TCRA imejikita kuelezea jambo lilotokea na hii ikiwa ni pamoja na kuelezea ni jinsi gani gharama za mawasiliano nchini bado zipo chini kulinganisha na wastani wa gharama duniani kote.
Je kuna lolote kubwa lilotolewa uamuzi?
• Imeagiza watoa huduma kuzingatia sheria kila wanapobadilisha bei za bidhaa zao;
(a) Kuziwasilisha kwa Mamlaka kabla hazijaanza kutumika,
(b) Kutoa taarifa za tozo za msingi na vifurushi kwa njia ambayo itaweza kuwafikia watumiaji wa simu za mkonini,
(c) Kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo haya na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo ( EPOCA (Tariff Regulation of 2011).
• Imewaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sio ya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko;
(a) TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja wao nafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji:
Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au mwezi ambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho wako tarari kulipia kwa mazungumzo, meseji na intaneti.
(b) Vifurushi vya mazungumzo tu: Hivi navyo kwa siku, siku saba au siku 30 kwa ajili ya watumiaji ambao hawahitaji intaneti na meseji kwa sababu moja au nyingine na wako tayari kulipia vifurushi vya sauti pekee;
(c) Vifurushi cha Meseji (SMS) tu: Kwa watumiaji ambao hawahitaji intaneti au muda wa mazungumzo kwa sababu moja au nyingine, au ambao wanatumia SMS kwa wingi. Hivi nayo viwe kwa siku, siku saba au siku 30 kwa bei ambazo mtumiaji atachagua.
(d) Vifurushi vya Intaneti tu: Kwa watumiaji ambao wanatumia intaneti kwa wingi. Hawa wapewe uhuru wa kuchagua vifurushi vya siku, siku saba au siku 30.
• inawashauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi yao. Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma. Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe malalamiko yake TCRA.
• Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huria la mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi chochote au huduma yoyote.
• Watumiaji wa simu janja zinazowezesha matumizi ya huduma nyingi, maarufu kama “smart phone”, kuwa makini wakati wa kuzitumia. Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia data hata kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenye vifurushi.
Je wewe unamaoni gani juu ya hili? Kumbuka unaweza kusoma taarifa nzima kutoka TCRA kwa kubofya hapa – TCRA (Faili ni la PDF)
Pia unaweza soma – Sababu za Mabadiliko kwa Gharama za Huduma ya Intaneti
No Comment! Be the first one.