Kwenye taarifa iliyotolewa leo na kampuni mama ya Tigo, Millicom imesema wamefanikiwa kuingia katika makubaliano na Vodacom kupitia huduma yao ya M-Pesa kuingia kwenye mfumo wa kuwawezesha wateja kutumiana pesa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti zao za pesa kwenye mitandao hiyo bila kupitia kwa wakala.
Mkataba wa kwanza wa namna hii ulifanyika mwezi wa sita mwaka jana kati ya Tigo, Artel na Zantel.
‘Kama wewe ni mteja wa M-Pesa na ukamtumia pesa mtu anayetumia huduma ya Tigo Pesa, pesa hiyo itaingia moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa na kitu hicho hicho kitakuwa kinatokea kama mtu wa Tigo Pesa akimtumia pesa mtumiaji wa M-Pesa. Hakuna utumiaji wa wakala kabisa.’
Kwa sasa mfumo uliopo ni kwamba kama mteja wa Tigo Pesa akimtumia pesa mtumiaji wa huduma ya M-Pesa basi mteja huyo wa Vodacom atapokea ujumbe mfupi ambao itambidi aupeleke kwa wakala wa Tigo Pesa ndani ya siku chache ili kuweza kupatiwa pesa zake.
Hii ni habari nzuri sana katika ukuaji zaidi wa sekta hii ya mawasiliano na kibenki.
Kusoma kuhusu mkataba wa kwanza uliounganisha Tigo, Airtel na Zantel Bofya Hapa!
Chanzo – Millicom.com
No Comment! Be the first one.