fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti

Blogger Wapiga Marufuku Blog za Ngono

Blogger Wapiga Marufuku Blog za Ngono

Spread the love

PrintHabari nzuri kwa ‘wote’ wasiopenda uwepo wa mitandao yenye video na picha za ngono kwa urahisi katika blogs za Google na pia ni habari mbaya kwa wote wanaomiliki au kutembelea blogs za namna hiyo zilizopo kwenye mfumo wa Blogger au maarufu kama blogspotDotCom.

Kampuni ya Google imetangaza ya kuwa kuanzia tarehe 23 mwezi wa 3 na kuendelea mitandao ya namna hiyo itakuwa maarufu kwenye huduma yao ya Blogs. Kama unamiliki tayari blog yenye picha au video za ngono basi itaondolewa kutoka kwenye kupatikana kwa watu wengine na mtandao huo utaweza kuifikia wewe tuu, na kama ukianzisha mtandao mpya baada ya tarehe hiyo basi mtandao huo utafungwa mara moja baada ya kugundulika na wametishia kumchukulia hatua mwanzilishi huyo.

SOMA PIA  Wachoma moto minara ya 5G kwa hofu ya kwamba 5G inasambaza Coronavirus

Kwa muda mrefu mtandao huo umeruhusu mitandao yaenye mambo ya ngono ifanye kazi kwa uhuru na wengi wameshtushwa na uamuzi huo. Wengine wakidai kampuni ya Google kuwa wanafiki kwa kujidai kupigania uhuru na kutokuwa madikiteta wakati uamuzi huu unawafanya kuwa kinyume na madai hayo. Uamuzi huu umechukuliwa na wengine hasa huko ulaya na amerika kama kitendo cha kudhibiti uhuru wa watu.

Wengi wanaona bloga wengi wataamia WordPress

Wengi wanaona bloga wengi wataamia WordPress

Wakati mtandao wa Google umeamua hivi, pia mtandao mwingine maarufu nchini Marekani wa Reddit.com nao umekuja na utaratibu kama huu. Kwa muda mrefu ni mtandao wa Facebook tuu ndio umekuwa ukishikilia na kutekeleza sheria kama hii. Mshindani mkubwa wa Blogger, mtandao wa WordPress hawakatazi watu kuanzisha blog za namna hii kama tuu utaratibu wa kuzitambulisha kama ni za kikubwa ukifuatwa. Inategemewa bloga wengi wa mambo ya kingono watahamia kwenye mtandao huo.

SOMA PIA  Tinder inashirikiana na Spotify kuzindua kipengele kipya cha 'Music Mode'

Tupe maoni yako, na kumbuka tunafurahi sana kila tunapoona mkizidi kusambaza makala zetu kwenye mitandao ya kijamii! Endelea kufanya hivyo, tusaidie tuzidi kukua na tuzidi kukuhabarisha na kukufundisha. Ungana nasi pia kupitia  Twitter, Facebook na Instagram

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania