fbpx
Intaneti

5G Marekani: Huduma ya 5G yaanza kupatikana rasmi nchini Marekani

majaribio-ya-5g-marekani
Sambaza

Teknolojia ya 5G Marekani imekuwa ni kitu kilichopata sifa ya usalama wa kitaifa. Ni teknolojia ambayo Marekani na mataifa mengine yanayoendelea yanaamini ni teknolojia muhimu sana kiusalama na kiuchumi katika kipindi hiki na miaka ya baadae.

Moja ya mtandao mkubwa nchini humo, Verizon, wafunga rasmi vituo vya kurusha huduma ya intaneti ya 5G katika miji miwili mikubwa nchini humo. Miji hiyo ni Chicago na Minneapolis. Hii ni miji mikubwa miwili, kati ya miji 30 nchini Marekani ambayo mtandao huu wa simu inataka kuweka huduma ya 5G kufikia mwisho wa mwaka.

INAYOHUSIANA  Nchini Ufilipino mitandao mbalimbali ya video za ngono yafungiwa

Je, kasi yake ikoje?

5g marekani
Wastani wa kasi ya 5G: Kwa sasa ni zaidi ya MB 400 kwa sekunde

Kwa sasa bado simu zinazokubali teknolojia hiyo ni chache, simu ya Motorola Moto Z3 ni moja ya simu inayopatikana na kuuzwa na mtandao huo na inakuja na teknolojia ya 5G. Kwa utumiaji wa simu hiyo waliojaribu kutumia teknolojia ya 5G wamepata wastani wa kati ya MB 400 hadi MB 700 za kasi ya ushushaji mafaili (Downloads). Verizon wamesema kasi inaweza kufika hadi GB1.

Teknolojia ya 5G ni ghali sana katika usambazaji kwani kwa sasa bado vifaa vyake haviwezi kusambaa eneo kubwa sana, hivyo usambazaji wa eneo kubwa linahusisha uwekaji wa vifaa vya urushaji 5G maeneo mengi zaidi. Hadi sasa kwa jiji la Chicago tu ndio Verizon wameweka huduma hiyo katika eneo la kilometa 50 za mraba, hii ni ndogo kwani mji mzima wa Chicago ni takribani Km 606 za mraba.

Kwenye sekta ya usalama inaaminika teknolojia hii itaboresha kwa kiasi kikubwa utumiaji wa vifaa kama vile ndege za kivita zisotumia rubani na pia roboti wa aina mbalimbali kwani wataweza kupokea na kutuma data kwa kasi kubwa.

roboti 5g
Teknolojia ya roboti anayeendeswa kutoka mbali kwa utumiaji wa teknolojia ya 5G roboti ataweza kupokea maamuzi haraka zaidi

Teknolojia ya 5G ya Huawei inasifika ya kuwa ya bei nafuu zaidi na pia inafika eneo kubwa zaidi ila tayari nchini Marekani imepigwa marufuku kutumiwa na huduma za mawasiliano nchini humo kwa sababu za kiusalama. Serikali ya Marekani haina imani na kampuni ya Huawei kiusalama/kijasusi.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kushusha "Search History" Yote Ya Google!

Wakati bado kwenye mataifa yetu yanayoendelea hata huduma ya 4G haijasambaa sana wenzetu wanapiga hatua zaidi vipi unamaoni gani? Tuambie kwenye eneo la komenti. Soma pia -> Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G, n.k

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |