fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao Mtandao wa Kijamii

FAMAHU: Wanaume Wengi Wanatumia App za Mahusiano Sana Kuliko Wanawake!

FAMAHU: Wanaume Wengi Wanatumia App za Mahusiano Sana Kuliko Wanawake!

Spread the love

android-dating-apps-640x469

Uchunguzi unaonyesha kuwa takribani watu milioni 90 ambao wanatumia App za mahusiano (Dating Apps) ambazo zinaonyesha maeneo (Locations) zao, kama vile Tinder na Momo mwezi uliopita. Na ikagundulika kuwa karibia robo tatu ya watumiaji ni wanaume.Kampuni ya utafiti ya GlobalWebIndex  imefanya utafiti katika nchi 32 na imepata taarifa kuwa 62% ya watumiaji wa App za mahusiano ni wanaume.

Habari hii sio ya kushangaza sana. Mwaka 2013, kituo cha uchunguzi ‘Pew Research Center‘ kiligundua kuwa wanaume ndio wako ‘active’ katika App na tovuti za Mahusiano. 13% ya wanaume wa Amerika wanatumia App na tovuti za mahusiano wakati 9% tuu ya wanawake ndio wanajihusisha na mambo hayo.

SOMA PIA  Twitter yatozwa faini ya $150m (bilioni 349 Tsh) kwa kuuza data ya watumiaji

dating_apps_best_apps_hero

Japokuwa hiyo haimaanishi wanume ndio wanatumia muda mwingi ndani ya App na tovuti hizo kulinganisha na wanawake. Mtandao wa Tinder ambao ‘New York Times‘ imeufanyia makasio/makadirio kuwa una zaidi ya watumiaji milioni 50 walioko ‘Active’. Wakati wanaume wanatumia wastani dakika 7.2 katika matumizi ya App, Wanawake wanatumia Wastani wa dakika 8.5 katika kutumia App hiyo.

Unachukuliaje App hizi? Je Zinajenga Au zinabomoa? Ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Twitter, Facebook Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania