Je unadhani unachoweka kwenye akaunti yako ya Instagram hakitakuja kukuletea matatizo? Muulize 50 Cent, inaonekana alivyoviweka kwenye mtandao huo havikuishia huko na sasa ameamua kujiweka pembeni.
Msanii wa muziki, 50 Cent, miezi michache iliyopita alikuwa amejitangaza kufirisika mahakani na hivyo kuiomba mahakama moja nchini Marekani kumuweka huru (kuchukuliwa kama mtu aliyefirisika) dhidi ya malipo mbalimbali aliyokuwa akiwa anadaiwa.
Lakini kutokana na uamuzi wake wa kuwa anapost picha mbalimbali katika mtandao wa Instagram huku akionesha pesa alizokuwa nazo alijikuta akiingia matatani na Mahakama hiyo. Na sasa ameamua kujiweka pembeni na kuachana na uendeshaji wa akaunti yake.
Amesema sio anatoka kwenye mtandao huo bali kuanzia sasa atamuachia mtu spesheli kusimamia akaunti hiyo. 50 Cent ni moja ya wasanii wakubwa waliokuwa wakiendesha akaunti zao bila msaada wowote.
Alipoulizwa na mahakama kuhusu pesa na mali anazoonesha katika akaunti yake ya Instagram alijitetea akisema si kila kitu anachopigwa picha nacho iwe nguo, pesa, gari au mali yeyote ni vya kwake – akisema amiliki kila kitu anachopigwa picha nacho. Na inasemekana kuna uwezekano mkubwa pesa hizo anazotumia nyingi zake ni feki.
Chanzo: BET