Noor Solar Complex ni mtambo wa kufua umeme unatokana na jua, mtambo huu utakapo kamilika utakuwa ndio mradi mkubwa zaidi duniani wa kufua umeme kwa njia hii na utakuwa unauwezo wa kusambaza umeme sehemu kubwa ya Afrika ya kaskazini.
Katika sekta ya nishati hivi sasa jicho limegeuziwa katika utafiti wa vyanzo vya nishati visivyo na madhara katika mazingira, vyanzo vingi vilivyopo sasa ni vyanzo ambavyo kwanza vitaisha lakini ni vingi sio rafiki sana na mazingira.
Hii ni moja ya sababu kwamba kumekuwa na pesa nyingi zinatumiwa katika tafiti za nishati mbadala, na mradi huu wa Noor solar complex ni moja ya mafanikio ya tafiti hizo.
Morocco imezindua hatua ya kwanza ya mradi huu wa umeme wa jua pembezoni mwa jangwa la sahara katika mji wa Ourrzazate, kwa hatua ya kwanza tu mradi huu unazalisha Megawati 160 ambazo zinakaribia zinazolishwa na bwawa la Kihansi (Tanzania) ambalo linatoa MW180.
Noor Solar Complex itajengwa katika hatua tatu, ya kwanza ndio hiyo imekamilika na hatua ya tatu inategemewa kukamilika mwaka 2018 na wakati huo mradi utakuwa umechukuwa karibu hekari 6000 na huku ukizalisha megawati 580 ambazo zaidi ya umeme unaozalishwa na Mabwawa ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Pangani, Hale na Nyumba ya Mungu yote ya Tanzania ambayo yanazalisha megawati 560.
Mradi huu sio kama miradi tuliyoizoea ya umeme wa nguvu za jua, mradi huu unatumia teknolojia ya kukusanya nguvu za jua ambazo zinatumika kuchemsha kimiminika fulani mpaka inafikia nyuzi joto 393 za Celsius na baada ya hapo kimiminika hiki kiatumika kuchemsha maji ambayo yanatoa mvuke ambao unatumika katika kuzungusha tabaini za kuzalisha umeme.
Mradi huu unasifa ya kipekee kwa kuwa unaweza kuzalisha umeme hata nyakati za usiku ambazo hakuna jua, ndiyo hii inawezekana kwa sababu kimiminika kinachochemshwa na jua mchana kinaweza kuhifadhi joto linalopatikana mchana na kulitumia nyakati za usiku na zile nyakati ambazo hazina jua.
Afrika Mashariki inayonafasi ya kujifunza kutoka kwa Morocco ambayo imetumia nafasi yake kijiografia kuweza kupata umeme, Afrika mashariki ipo katika eneo la ikweta ambalo linapata jua kwa muda mrefu zaidi kuliko maeneo ya pembe ya dunia hivyo inanafasi kubwa ya kunufaika na umeme wa jua.
One Comment
Comments are closed.