Bilionea mjasiriamali, Elon Musk huenda akafanya hadithi za kusadikika kutoka kwenye vitabu vya sayansi kuwa kweli, kwa kuwezesha binadamu kusafiri kwa haraka zaidi ndani ya bomba lililopunguzwa hewa kabisa (vacuum) zinazoweza kwenda kwa spidi kubwa zaidi ya ile ya ndege. Bomba ilo pamoja na vyombo vyake vya usafiri kufahamika kama Hyperloop.
Ujenzi wa majaribio wa bomba hilo huenda ukaanza kufanyika mapema mwakani, na majaribio ya mwanzo kutazamiwa kufanyika katika bonde la Quay, huko Califonia mwaka 2018 na kugharimu Dola Milioni 100 kwa kuanzia.
Kampuni ya Hyperloop Transportation Technologies wanataka kuthibitishioa dunia kuwa hilo linawezekana, kwa kuingia ubia na mashirika mengine kama kampuni ya ubunifu wa ukandarasi ya AECOM na Shirika la Uswisi la Oerlikon ambalo limejikita katika teknolojia za utupu (Vacuum-technology) ambao ndio mhimili wa mradi huu.
Mtandao maarufu wa teknolojia wa Wired, ulioripoti kuhusu mwanzo wa mradi huu kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Dhana ya mwanzo ya mradi huo inaonyesha ganda la nje, mfano wa gari dogo lenye siti za abiria likiwa ndani ya bomba(tube) ya aluminiam. Nguvu ya umeme itatumika kuendesha usafiri huu. Kwa usafiri huu, umbali wa Kilomita hadi 600 (Karibu na Umbali wa Arusha hadi Dar es Salaam) huenda ukafikiwa kwa muda wa NUSU saa tu! Ndio, Nusu saa tu.
Mkufunzi mmoja wa mambo ya usafiri amesema huenda mradi huu ukabakia kuwa dhana kutokana na vikwazo kama milima pamoja na gharama.
Musk mwenyewe amesema amejikita zaidi katika mradi wa majaribio, na amesisitiza kuwa utakuwa wa wazi kwa yeyote atakayekuwa tayari kutaka kuuendeleza.
Vyanzo; Al-Jazeera, TheStar.com, ETE na Google Images
No Comment! Be the first one.