Kampuni nguli kutoka China ya Huawei imetangaza simu ambayo ina kamera ya aina yake. Simu hii kwa Huawei ni ya kwanza yenye mfumo huu wa kamera. Kamera yake inazunguka nyuzi 180 na pia ina MP (Mega Pixels) 13.
Hii inamaanisha kuwa kamera yake ya selfie (mbele) ni mega pixel 13 na hata ile ya nyuma ni mega pixel 13 pia. Wale wa selfie hapa ndipo patamu. Kwa App kwa Snapchat na Instagram simu hii inafaa sana kwa sababu inatoa selfies makini sana zenye ubora wa hali ya juu.
Kwa kulinganisha na iPhone 6 ambbayo ina mega pixel 1.2 kwa kamera yake ya mbele na hata Samsung galaxy s6 Edge yenye Mega pixels 5 kwa kamera ya mbele bado simu hii (Huawei Honor 7i) bado ipo juu.
Kamera katika Honor 7i ina sensa inayojulikana kama ‘Sony Exmor sensor’ na pia ina flash. Hii inasaidia pale watumiaji wanapoizungusha kwa lengo la kupiga selfie, kupata selfie yenye mwanga wa kutosha (Pia yenye kiwango)
HUAWEI HONOR 7i INAJENGWA NA YAFUATAYO
- Huawei Hoor 7i ina kioo cha inchi 5.2 ambayo ina ‘resolution’ 1080p.
- Ina prosesa ya Qualcomm’s Snapdragon 616, RAM 2GB
- Inaweza ingiza memori kadi ya microSDVX hadi 32GB kama ujazo wa nyongeza
- Simu janja hii inaendeshwa na Huawei EMUI 3.1 ambayo ni program endeshaji iliyojikita katika Android Lollipop 5.1
- Ina uwezo wa Bluetooth, WiFi, na hata GPS
- Uwezo wa Honor 7i katika betri ni 3,090 mAh
- Pia ina sensa ya sahihi ya kidole (Finger print) ambayo ipo katika upande wa simu
Huawei Honor 7i itauzwa china kwa dola za kimarekani 250 tuu lakini kwa sehemu zingine duniani itakua ikiuzwa kati ya dola za kimarekani 300 mpaka 400 –Nyumbani kupewa kipaumbele kwanza–
No Comment! Be the first one.