Watumiaji wa simu za Apple ambao wanatumia iPhone 6 Plus ambazo zina matatizo ya kamera yaani kamera inakua inatoa picha zenye ukungu (blurry) kidogo. Kama matatizo hayo yanakukumba huu unaweza ukawa ndio msaada juu ya simu yako hiyo.
Apple wameanzisha programu mahususi inayoitwa ‘iSight Camera Replacement Program’ baada ya kampuni kuona kuwa kuna baadhi ya simu ambazo walizalisha zenye matatizo hayo ya kamera. Matatizo hayo yanafanya picha ambazo zimepigwa na baadhi ya iPhone 6 plus kutokuwa na hadhi inayostahili.
Baadhi ya simu hizo ni zile zenye namba za utambuzi (serial number) ambao zilitengenezwa katika mwezi septemba 2014 mpaka januari 2015
Watumiaji ambao wame(na)kutana na matatizo haya inawabidi waingie hapa katika mtandao maalumu ambao umejikita katika kutatau tatizo hilo la simu za iPhone 6 Plus katika kamera ambazo zinatoa ukungu (blurry) katika kupiga picha
Katika mtandao huo watumiaji wa iPhone 6 plus hizo wanaweza ingiza namba za utambulisho wa simu zao (serial number) ili kutambua kama simu zao zipo katiki zile simu ambazo zina matatizo hayo (zile za septemba 2014 mpaka januari 2015). Apple wamesema kama mtumiaji wa simu hiyo anataka kujiunga na programu hii basi simu yake (iPhone 6 Plus) inabidi iwe katika hali ya kufanya kazi yaani isiwe mbovu. Kama serial namba ya simu ipo katika zile za kati ya septemba na januari basi kampuni ya apple litafanya marekebisho ya kamera hiyo bure
Watumiaji wa simu ambao watajikuta namba za utambulisho wa simu zao zippo katika pprogramu hiyo itawabidi wachague namba ambavyo simu zao zinaweza kutegenezwa kamera katika machaguo matatu. chaguo la kwanza ni Kuipeleka simu hiyo kwa mtoa huduma aliethibitishwa na Apple, Chagua la pili ni kupanga muda wa kuonana (Appointment) na duka la mauzo la Apple na chaguo la tatu (la Mwisho) ni Kuwasiliana na Apple kitengo cha ufundi mwenye simu aweze kuelezewa jinsi amabavyo kamera hiyo inavyowezwa kurekebishwa.
Apple pia wameweka wazi kuwa kabla ya mtu kutuma simu yake ikafanyiwe marekebisho hayo basi hana budi ku back up taarifa zake zote katika kompyuta yake kisha ndio aitume
Pia Kwa wale ambao iPhone 6 plus zao zina matatizo kama vile ya kioo kupata nyufa inabadi warekebishe kwanza matatizo hayo kabla ya kutuma simu zao au kama wakiamua kutuma hivyo hivyo kutakua na gharama za ziada ili kuwezesha kutengeneza kwa vioo hivyoo
No Comment! Be the first one.