Kifaa cha kupima malaria bila ya damu chaundwa nchini Uganda

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 24, Brian Gitta, raia wa Uganda ameshinda zawadi ya mvumbuzi bora inayotolewa kila mwaka na Chuo cha taaluma ya Uhandisi (Royal Academy of Engineering Africa prize) cha nchini Uingereza.

Brian Gitta amepata tuzo hiyo baada ya kuunda kifaa kwa ajili ya kupima na kutambua ugonjwa wa malaria bila ya kutumia damu ya mgonjwa kama ilivyo desturi ya maabara.

INAYOHUSIANA  Fahamu: Simu Janja 1000 zinaingia Sokoni kwa Kila Sekunde 21.8

Gitta pamoja na wenzake, wametengeza kifaa kidogo ambacho hakiihitaji utaalam katika kukitumia ambapo chenyewe humhitaji mgonjwa kukiweka kwenye kidole chake.

kifaa cha kupima malaria

Kifaa hicho kilichopewa jina la Kiswahili, ‘Mattibabu’ kimefanyiwa majaribio na kuonesha kwa asilimia 80 kinatoa majibu sahihi ya kutambua malaria kwa mgonjwa.

Kwa namna kilivyotengenezwa hutambua mabadiliko ya maumbo, rangi pamoja na wingi wa chembe hai nyekundu za damu ambazo zimeathirika kwa malaria. Majibu yanapatikana ndani ya dakika moja kupitia simu ya mkononi inayounganishwa na kifaa hicho.

INAYOHUSIANA  Wapenzi 20 na iPhone 7 ishirini vyawezesha Mchina kununua nyumba

Lakini Gitta na timu yake wamekuwa wakiboresha kifaa hicho na wana uhakika kwamba majaribio mapya yatakuwa ni majibu sahihi kwa asilimia 90 ya kutambua ugonjwa wa malaria.

kifaa cha kupima malaria

Brian Gitta akiwa na kifaa cha kupima malaria, ‘Mattibabu’.

Kufanyia majaribio ya kifaa hicho wanashirikiana na hospitali za kidhaa nchini Uganda. Lengo kubwa likwa ni kuwezesha Mattibabu kupatikana kwa watu binafsi, maabara, vituo vya afya na hospitalini.

Kupitia tuzo hizo watafiti wa kimataifa watakifanyia majaribio kifaa hicho na kutoa ripoti mwezi ujao kuhusu uwezo wa ‘Mattibabu’ katika kubaini mgonjwa anasumbuliwa na malaria.

Kwa ushindi huo, Gitta amezawadiwa fedha taslimu pauni za Uingereza 25,000|zaidi ya Tsh. 76m katika sherehe zilizofanyika mwezi huu Nairobi, Kenya.

Royal Academy of Engineering Africa prize ndio tuzo kubwa zaidi kwa Afrika inayotolewa kwa wahandisi wabunifu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.