Apple washika namba moja kimauzo robo ya mwisho ya 2020, Huawei waporomoka sana
Apple washika namba moja kimauzo katika sekta ya simu janja katika robo ya mwisho ya mwaka 2020. Hii ni kutokana na data mpya za kimasoko kutoka shirika la Gartner.
Apple washika namba moja kimauzo katika sekta ya simu janja katika robo ya mwisho ya mwaka 2020. Hii ni kutokana na data mpya za kimasoko kutoka shirika la Gartner.
Marekani yaweka vikwazo zaidi kwa Huawei. Katika hatua za mwisho zilizochukuliwa na Rais Trump dhidi ya Huawei ni kuwanyima uwezo wa kununua prosesa za Intel, hii ikiwa na vikwazo vingine kadhaa.
AppGallery ni soko la Apps linalomilikiwa na Huawei, linaendelea kuboreshwa huku likiwa linaendelea kupata mamilioni ya watumiaji.
Uongozi wa Rais Trump umeiweka kampuni ya Xiaomi katika vikwazo vya kibiashara kwa kuiweka kwenye orodha ya makampuni na biashara ambazo watu na makampuni ya kimarekani hawaruhusiwi kuwekeza.
Baada ya miezi kadhaa ya kukata mahusiano na kampuni ya Huawei, brand ya Honor kuja na laptops zinazotumia programu endeshaji ya Windows 10. Hii ni baada ya kukamilika kwa mikataba ya kibiashara na kampuni ya Microsoft.
Kukamilika kwa kiwanda cha Chip cha Huawei cha kwanza nchini China ni ishara kubwa ya uamuzi wao wa kuhakikisha wanajitegemea katika teknolojia muhimu za utengenezaji simu.
Je ushawahi jiuliza chipset ni nini kwenye simu n.k.? Chipset ni moja ya kiungo muhimu kwenye simu janja yako. Ni kitu kinachowezesha simu yako iwezo kufanya kazi zake za kitofauti tofauti kwa ufanisi mkubwa – bila kutumia chaji nyingi sana, kutochukua nafasi kubwa ndani ya utengenezaji wa simu na faida nyingine nyingi.
Biashara ya utengenezaji na uuzaji wa simu za Honor imeuzwa na kampuni ya Huawei. Kuanzia sasa simu zinazobeba jina hilo hazitatengenezwa wala kuuzwa na kampuni ya Huawei.
Huawei wamekuwa kazini kwa miezi kadhaa wakitengeneza programu endeshaji ya ziada dhidi ya Android. Na sasa ni rasmi programu endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya kutumika kwenye simu kufikia Disemba mwaka huu.
Simu ya Huawei Y5 Prime toleo la 2018 ni moja ya simu ya bei nafuu kutoka kwa kampuni ya Huawei. Huawei kwa sasa bado wako katika kifungo cha matumizi ya huduma za Google (Google Play Services), app na huduma zingine nyingi za makampuni ya Ulaya na Marekani lakini kwa simu hii bado hali ni tofauti.
Huawei wazidi kuporomoka kimauzo katika soko la uuzaji simu duniani. Data zinaonesha Samsung wakizidi kulishika soko huku Huawei mambo yakienda tofauti kwao.
Huawei wataendelea kutengeneza simu bila huduma za Google kwenye simu zake hadi mwaka 2021, mwezi Mei.
Mwaka 2020 umekuwa na mengi lakini kubwa zaidi ni kuhusu virusi vya Corona ambavyo vimeyumbisha uchumi wa Dunia kwa asilimia kubwa tuu; kuhusu kiasi gani cha simu zimefika sokoni simu huko ni huzuni!.
Hivi karibuni Huawei ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Duka lake la programu la AppGallery litakalokuwa kwenye simu zake za Huawei. Taarifa kutoka Huawei zinasema AppGallery ya sasa limekuwa duka kubwa la tatu duniani baada ya Android(Play store) na Apple (App store).
Makampuni nguli kutoka China yaani Huawei, Oppo, Vivo, na Xiaomi ambayo yapo vizuri katika teknolojia za utengenezaji wa simu janja, yameunganisha nguvu katika kuja na mbadala wa soko la apps la #Google PlayStore.
Kampuni ya simu ya Huawei ipo katika mpango wa kuhakikisha simu zake mpya kuja na apps 70 maarufu ili kuepuka vikwazo vya serikali ya Marekani vinavyowazuia kutumia huduma za Google ikiwa ni pamoja na soko la apps la Google PlayStore.
Huduma ya Intaneti yenye kasi zaidi ya teknolojia ya 5G imeanza kutolewa na mashirika ya mawasiliano ya simu nchini China katika zaidi ya miji 50.
Samsung wafunga kiwanda nchini China. Kampuni hiyo inayoshikilia namba moja katika utengenezaji na uuzaji wa simu janja duniani, imefunga kiwanda chao pekee nchini China kwa ajili ya utengenezaji wa simu.
5G yaanza kupatikana katika nchi ya kwanza Afrika. Baada ya ‘figisu figisu’ za mataifa ya Marekani na baadhi ya washirika wake wa ‘kuibania’ kampuni ya Huawei juu ya usambazaji wa teknolojia yake ya kisasa zaidi ya mtandao wa 5G, kampuni hiyo imepeleka teknoljia hiyo nchi ya Afrika Kusini.
Kampuni ya Huawei yatambulisha rasmi toleo lao la simu janja za hadhi ya juu za Huawei Mate 30 na Mate 30 Pro, ingawa zinakuja na teknolojia za kisasa hii ikiwa ni pamoja na 5G ila haziji na uwezo wa kuwa na apps maarufu za Google.