Huawei ni kampuni kubwa sana duniani inayojihusisha na maswala ya teknolojia, kwa sasa wamekuja na mashindano ya TEHAMA.
Katika mashindano haya tunawakilishwa na wanafunzi kutoka katika chuo kikuu cha Dodoma na chuo kikukuu cha Dar es salaam.
Haya yakiwa ni mashindano yaliyoandaliwa mahususi kwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara. NA hatua hii ni ya fainali katika mashindano hayo.
Hatua za mwanzo mwanzo kabisa katika mashindano hayo watanzania waliibuka kidedea kwa kupata nafasi za juu kabisa yaaani nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu.
Hiyo ilikua ni kwa kanda ya kusini mwa afrika, huku kanda zingine zikichuana na kupata washindi ambao ni wawakilishi wao katika fainali hizi.
Mashindano haya yatafanyika kwa njia ya mtandao tarehe 18.06.2022. TeknoKona hatuna budi kuwatakia kila lenye kheri katika mashindano hayo
Tutajivunia sana kuona wanaibuka kuwa washinda katika mashindani haya, Ukaingalia kwa upande mwingine ni kwamba inatia hamasa kubwa kuona tuna washiriki katika nafasi ya fainali kutoka kwa vijana wa chuo kikuu.
Kumbuka Tanzania kuna watu mbali mbali na wanajihusisha na maswala makubwa tuu ya kiteknolojia lakini mara nyingi huwa hawaonekani au hawapati sapoti kutoka kwa wadau mbali mbali.
Kumbuka pia shindano hili la Huawei ni moja kati ya mashindano makubwa sana maana katika hili tuu limeweza kushirikisha nchi Zaidi ya 85 duniani kote na vyuo Zaidi ya 200 huku wanafunzi 150,000 wakiwa wanachuana.
Tujivunie cha kwetu!
CHANZO: IPP MEDIA
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa commnet, je hili umelipokeaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.