Ni wazi kwamba ili simu janja ikamilike mara nyingi huwa vinachukuliwa vifaa vya kampuni mbalimbali na kuunganishwa ila kuunda simu janja lakini Huawei ni moja kati ya makampuni yanayopunguza adha hii.
Huawei ni moja kati ya makampuni ya kiteknolojai ambayo yanapokea vizingiti vingi ila bado kamapuni inapambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa inawaletea wateja wake teknolojia bora zaidi.
Chip (Chipset) ndio huwa inaunganisha na kusafirisha taarifa kutoka kwenye ubongo wa kifaa (CPU), Kumbukumbu ya kifaa n.k na kisha kuzipeleka katika maeneo mbalimbali katika sakiti (circuit) ya kifaa hicho.
Kwa haraka haraka ni kwamba yenyewe ndio inapeleka taarifa kwa mpangali unaotakiwa kutoka eneo moja kwenda nyingine….au fanya hivi soma zaidi >>HAPA<<
Hii inamaana chip nzuri itarahisisha ufanisi katika kifaa chako, mfano Qualcomm ni moja kati ya makampuni ambayo yanasifiwa sana katika kutengeneza chip nzuri ukilinganisha na mengine mengi na wateja wake ni kama kampuni ya Apple.
Huawei wameona nao wasibaki nyuma na kutegemea chip kutoka katika makampuni mengine na kwa sasa wako katika hatua za mwanzo katika kuhakikisha kuwa wanakuja na Chip yao wenyewe.
Hatua hizi za mwanzo zinahusisha hata majaribio mengi kwa sasa ili kuhakikisha kuwa wanakuja na chip bora kabisa ambazo pia wanaweza kuziweka katika simu zao na hata kufanya biashara ya kuziuza.
Kwa sasa Huawei hawajaweka wazi kwamba pengine ni lini na ni vifaa gani vitakua vinatumia chip hizi.
Kwa Huawei hii ni habari nzuri maana ukiwa na uwezo wa kutengeneza na kutumia cha kwako ni vizuri sana kuliko ukiwa unanunua kwa mwingine sio?
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani kampuni itaweza kushindana na makampuni mengine makabwa ambayo tayari yapo katika soko la aina hiyo? Niandikie hapo chini katika uwanja wa comment .
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.