Katika programu endeshi kubwa hivi sasa HarmonyOS ni miongoni mwao ambao hadi sasa imeshafikisha watumiaji milioni 70 huku namba hiyo ikitarajiwa kusogea mara dufu.
Habari za HarmonyOS zilianza kuvuma mwaka 2019 wakati na dunia ikafahamu kuwa Huawei wanajipanga kuja na kitu chao wenyewe kwenye ulimwengu wa teknolojia ambao haukaukiwi ushindani kila sekunde inayopita. Juni, 2 2021 ndio programu hii endeshi ilipelekwa kwa baadhi ya vifaa vya kidijiti vya Huawei.
Simu janja ngapi za Huawei zimepelekewa taarifa ya kuhamia kwenye programu endeshi mpya?
Kwa miezi kadhaa sasa zimekuwepo taarifa kuwa simu janja mbalimbali za Huaewei zitapelekwa taarifa fupi ya kuweza kuhamia kwenye programu hiyo endeshi mpya ambapo hadi sasa zaidi ya rununu za Huawei 100 milioni zimeingizwa kwenye mpango wa kupakua masasisho hayo ambapo mtumiaji wa simu janja ataweza kuhama kutoka kwenye Android na kuanza kutumia HarmonyOS 2.0.
Safari ya kundi la kwanza kuhamia kwenye HarmonyOS ilianza Juni 2 mwaka huu na chini ya miezi mitatu imeweza kuwafikia watumiaji 70 milioni wanaotumia Huawei na Honor nchini Uchina pekee.
Wakati wa uzinduzi wa programu endeshi Mtendaji Mkuu wa Huawei alahidi vifaa vya kidijitali 100 milioni vitaweza kuhamia huko kwenye toleo hilo.
Programu hii endeshi imepelekwa kwenye simu janja chache sana duniani kote. Je, wewe unatumia programu endeshi kwenye simu yako?
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.