Huawei ambao wamekuwa wakipeleka programu endeshi ya kwao kwenye simu janja nyingi zaidi wanatazamiwa kufanya uzinduzi wa bidhaa mbalimbali mnamo Oktoba 21 ya mwaka huu.
Katika uzinduzi huo ambao utafanyika Vienna-Austria saa 10 jioni saa za Afrika Mashariki na Bw. Derek Yu-Rais wa Mashariki ya kati ya Ulaya, Ulaya Kaskazini na Canada chini ya mwamvuli wa Huawei. Huawei wanatazania kuzindia bidhaa lakini lakini hajawaweka wazi ni vitu gani ambavyo vitatambushwa.
Kwa mujibu wa mwaliko waliupata GSMArena, umebainisha kuwa moja ya bidhaa ambazo zitazinduliwa siku hiyo ni simu janja lakini haijajulikana ni ipi. Hata hivyo, kulingana na vyanzo mbalimbali inaelezwa simu janja Huawei P50 iliyotambulishwa kwa mara ya kwanza mwezi Julai mwaka huu huko Uchina pengine sasa italetwa kwa wateja wa dunia nzima.
Mbali na Huawei P50 na 50 Pro kuanza kupatikana kwa wateja wengine duniani kote pia inatazamia Nova 9 nayo itafuata mkondo huo huku ikitazamiwa kutambulishwa Septemba 29 mwaka huu.
Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba Huawei P50 na P50 Pro zote zina kamera zenye MP 50 lakini kwenye upande wa kipuri mama moja ina Snapdragon 888 SoC (P50) huku nyingine ikiwa na Kirin 9000 (P50 Pro). Endelea kuwa nasi kwani tutaleta uchambuzi wa simu hizi mbili.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.