Kwenye ulimwengu wa simu janja ni vigumu kutoitaja Huawei na hii inatokana na rununu ambazo wamekuwa wakizitoa kwa miaka tuu na bado safari yao inaendelea. Hivi karibuni walizindua Huawei Nova 8 SE ambayo yenyewe ni ya 4G.
Kwa miaka ya karibuni Huawei imekuwa ikipitia kipindi kigumu kibiashara kwenye mataifa mengi duniani lakini hilo halijawafanya waachane na biashara ya simu janja hata kama wanapata hasara ama kwa lugha nyingine mauzo yao yanashuka. Bado tunaendelea kuiona Huawei kwenye biashara hivyo si vibaya tukafahamu sifa za ndani kuhusu Nova 8 SE 4G.
Muonekano|Kipuri mama
Kwa muonekano Huawei wanakwenda na ushindani uliopo sokoni kwa lengo la kwenda sambamba na kile ambacho kwa sasa kinapendwa zaidi na watumiaji. Huawei Nova 8 SE ni simu janja yenye kioo cha chenye urefu wa inchi 6.5 cha ung’avu wa hali ya juu; ubora wa OLED. Kipuri mama kilichowekwa kwenye simu hii ni Kirin 710A ambacho kina uwezo mkubwa tuu kuwezesha ufanisi wa 4G ndani ya rununu husika.
Memori|Kamera
Uwezo wa kuhifadhi vitu kwa maana ya memori kwenye simu hii unaridhisha na unavutia pia kwani RAM ni GB 8 huku diski uhifadhi ni 128 GB na kwa kwenda mbali zaidi ni kwamba haina sehemu ya kuweka memori ya ziada. Kwenye upande wa kamera nyuma zipo nne 4-MP 64, MP 8 na mbili zina MP 2 kila moja. Kamra ya mbele ina MP 16.

Uwezo wa betri|Mengineyo
Simu janja kuwa na uwezo kuchaji kwa teknolojia ya haraka ni kitu ambacho kimeonekana kukumbatiwa na makampuni mengi. Simu hii ambayo nimeileta mbel ya macho yenu katika mtindo wa maandhi ina 66W na betri lake lina 3800mAh. Uzito wake ni gramu 180, inatumia Bluetooth 5.1, WiFi, USB-C, USB OTG, inapatikana katika rangi nne ambazo zikiwemo Nyeusi, Fedha, Bluu.

Bei ya simu hii inakaribia $327| zaidi ya Tsh. 753,408 ambapo upatikanaji wake unategemewa kuanzia Disemba 10. Tunakaribisha maoni yako na usiache kutufuatilia kila siku.
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.