Moja kati ya vitu ambavyo vinasumbua mataifa mengi siku hizi kwenye suala zima la teknolojia ni udukuzi. Tafiti za hivi karibuni kuna uwezekano mkubwa wa drones kuweza kudukuliwa.
Drones hizi zimetengenezwa kwa kutumia programu ambazo zinakuwa zinaamriwa nini cha kufanya kutokana na amri iliyopewa lakini kwa tafiti mbalimbali zimeeleza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumia katika kudukua drones.
Drones ni ndege zinaondeshwa kwa kutumia kompyuta kwa maana nyinyine zinaendeshwa bila uwepo wa rubani. Kwa jina lingine unaweza ukaziita “Kompyuta zinazopaa“.
Kwa mfano “Maldrone” ni aina ya kirusi ambacho kinaweza kudukua drones kwa njia ya intaneti. Drones zimeonekana kupendwa na mataifa mengi kutoka Magharibi kwa sababu zimepunguza ulazima wa ndege kuendeshwa na rubani na badala yake kazi hiyo kufanywa na kompyuta.
Kudukuliwa kwa ndege hizo kunaweza kuleta madhara kama ambavyo unaweza kupata pale ambapo kompyuta/simu janja yako kuduliwa. Moja ya tafiti zilizofanyika njia kadhaa amabzo zinaweza kutumika kudukuliwa kwa drones.
Mojawapo ya njia zilizotumika ni pale timu ya watafiti walipoweza kutuma commands za uwongo kutoka kwenye laptop kwenda kwenye drone na kuifanya ianguke ardhini.
Kesi nyingine ya drone kudukuliwa ni pale mmoja kutoka kwenye timu ya watafiti alipotuma maombi ya kuunganisha kwenye mtandao wa drone kitu kilichosababisha processor ya drone kuzidiwa nguvu na hivyo kutua bila matarajio.
Tuambie maoni yako juu ya makala hii kwa kuandika comment yako hapo chini na usiache kufuatilia TeknoKona kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.
Vyanzo: Live Technology, Rocativ
One Comment
Comments are closed.