fbpx
Barua pepe, Intaneti, Maujanja, Teknolojia, Video

Njia rahisi ya kutuma kitu kupitia intaneti

kutuma-kitu-kikubwa-kupitia-intaneti
Sambaza

Kwa jinsi teknolojia ilivyokuwa na inavyozidi kukua si kitu cha ajabu kuona mtu akatumia picha jongefu kutoka mtandao wowote na kujifunza jambo fulani bila ya kupata msaada wa ana kwa ana.

Mara nyingi wengi wetu tumekuwa tukipata changamoto sana pale tunapotaka kumtumia mtu picha mnato ambayo ni kubwa kuliko kikomo kilichowekwa kulingana na programu tumishi unayotaka kutumia kufanikisha suala hilo.

INAYOHUSIANA  Betri kubwa duniani yazinduliwa; Musk atimiza ahadi yake

Mathalani kwa wale ambao tunatumia mawasiliano kwa njia ya barua pepe tunafahamu kabisa iwapo tukitaka kutuma kitu kinachozidi MB 25 basi itatubidi kutuma kupitia Google Drive, Outlook Drive, n.k.

Katika kuhangaika huku na kule kutafuta mbadala nikafanikiwa kufahamu tovuti ambayo inaruhusu kuambatanisha kitu/vitu ambavyo vina ukubwa wa kufikia GB 2.

Hutahitaji kujisajili ili kuweza kufanikisha adhma yako isipokuwa tu utaweka barua pepe ya mtu/watu ambao unataka kuwatumia bila kusahau kuweka na ya kwako kisha inakuwa tayari kumfikia mhusika. Bofya HAPA kujaribu kutuma kitu kwa mtu.

kutuma kitu
Muonekano wa tovuti ya WeTransfer.

Unaweza pia ukamtumia mtu kitu kupitia programu tumishi ya Telegram ingawa watu wengi hawajui lakini kwa maoni yangu Telegram ni bora zaidi kutokana na kutokuwa na ukomo wa ukubwa kuhusu kutuma kitu.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|