Kampuni za Huawei na Samsung zikiwa katika vita ya kuwa kampuni ya kwanza kutoa simu ya rununu ya mkunjo, mkurugenzi wa Huawei Ken Hun amethibitisha kwamba simu ya kwanza ya mkunjo na teknolojia ya 5G.
Aidha amesema wanatarajia simu hiyo itazinduliwa katikati ya mwaka 2019 ikiwa na teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G pamoja na simu yenye uwezo wa kukunjwa na kukunjuliwa lakini pia ikiwa na kioo kipana ambacho wanalenga watu kuacha kutumia kompyuta.
Mbali na kuwa na mipango ya kuzindua simu yenye 5G pia wanatarajia kuzindua Modem ya 5G mwishoni mwa mwaka huu.