fbpx

Kuingia sokoni kwa BlackBerry Evolve

0

Sambaza

Wakati wa uzinduzi wa simu/bidhaa fulani sio kwamba baada tuu ya shughuli hiyo kukamilika basi utaweza kuinunua, mara nyingi kama si wakati wote tarehe rasmi hupangwa ya kuanza kuuzwa au kwa lugha rahisi kuingia sokoni.

Mapema mwezi Agosti 2018 tuliweza kuleta mbele ya uso wa wasomaji wetu kuhusu undani (sifa) wa simu rununu mbili kutoka BlackBerry nikimaanisha BlackBerry Evolve na Evolve X.

Simu hiyo ilikuwa gumzo kwenye tovuti mbalimbali kwa sababu kuu mbili; kuwa simu za kwanza kutoka BackBerry bila ya kuwa na kicharazio (ina kioo cha mguso tu) na bei yake ni ya kuhimilika.

BlackBerry Evolve itaingia sokoni Okt. 10 2018 tofauti na ilivyokuwa ikitegemewa hapo awali (kuingia sokoni mwezi Septemba).

Kuingia sokoni

BlackBerry Evolve

BlackBerry Evolve iimewekwa kwenye kundi la simu ambazo si ghali sana, bei yake inafika karibu $350|Tsh. 805,000 kupitia Amazon pamoja na masoko mengine.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Oreo yafika kwenye Samsung Galaxy J7 Prime
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.