Ni miaka miwili imeshapita tangia toleo la mwisho la Huawei Mate kutoka, Mwaka huu mwezi septemba Huawei itatambulisha rasmi Mate 50.
Huu ni mwendelezo wa matoeo ya Mate ambayo ni matoleo ya juu kabisa katika kampuni ya Huawei na jina lake mara nyingi huwa linajiendesha lenyewe.
Ukiachana na baadhi ya vikwazo ambayo kampuni ilikutana navyo kama vile kuzililiwa katika baadhi ya masoko kama vile marekani n.k bado kampuni inajitahidi katika soko la simu janja.
Inafahamika wazi kwamba kwa sasa kampuni ya Huawei haitumii kabisa programu endeshi kutoka Android na pia hata soko la App la PlayStore.
Hivyo kwa sasa Huawei inajitegemea kwa kila kitu, soma Zaidi kuhusiana na mambo ya Samsung >>HAPA<<
Toleo la mate 40 lilizinduliwa rasmi mwaka 2020 mwezi oktoba na mpaka sasa imeshapitia miaka miwili, tusubiri mwezi septemba mwaka huu ili simu itangazwe rasmi.
Kwa sasa hakuna mambo mengi ambayo yanaelezea uwezo wa simu hiyo na vyanzo vingi vinasubiria simu hiyo itangazwe kwanza ili kujua ni vitu gani vitakua vikipatikana ndani ya simu hiyo.
Kumbuka kwa mwezi Septemba huo huo simu za iPhone 14 zinategemewa kutoka na vyanzo mbali mbali vinaeleza kuwa itakua na vipengele vya aina yake.
Ningependa kusikia kutoka kwako je unadhani simu hii itakua ni moja kati ya zile ambazo zinaleta ushindani mkumbwa katika soko la simu janja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.