fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps HarmonyOS Teknolojia

HarmonyOS yafikisha watumiaji 90 milioni

HarmonyOS yafikisha watumiaji 90 milioni

Spread the love

Programu endeshi (HarmonyOS 2.0) ambayo haijafikisha hata miezi mitatu tangu ipelekwe kwa wateja imeendelea kupaa kwa maana ya kuwafikia watumiaji wengi kwa kasi ambayo haikutegemewa; hivi sasa tunaongelea simu janja 90 milioni.

Huawei ambao wanajivunia na kuwa cha kwao wenyewe lakini pia kuleta ushindani kwenye upqnde wa programu endeshi wameendelea kuipeleka HarmonyOS 2.0 kwenye simu janja nyingi zaidi ambapo hivi sasa takwimu zinaonyesha kwa wastani ni watumiaji 8 kwa sekunde wanahamia kwenye programu hiyo endeshi.

Mapema mwezi Juni HarmonyOS 2.0 ilikuwa na watumiaji 10 milioni, 70 milioni (Agosti) na chini ya wiki moja baadae imefikisha watumiaji 90 milioni.

90 milioni

Sura ya HarmonyOS 2.0 kwenye simu janja.

Wachunguzi wanasema mwanzoni mwa mwezi Agosti takwimu zilionyesha takribani simu janja za Huawei/Honor zilikuwa zimekidhi kuweza kuhasmia kwenye toleo hilo la programu endeshi na mpaka mwisho wa mwezi namba zilikuwa zinakaribia rununu karibu 100 milioni.

Huawei haijaweka wazi kuhusu takwimu hizo ni simu janja ambazo zinahamia kutoka Android kwenda HarmonyOS 2.0 na iwapo rununu hizo ni Huawei za zamani ama ni vile ambazo zinatoka zikiwa tayari na toleo hilo la programu endeshi.

Mipango iliyopo ni kufikia vifaa takribani milioni 100 katika siku 100, 300 milioni mpaka mwisho wa mwaka huu na kwa kasi wanayokwenda nayo huenda wakafikia malengo yao waliyojiwekea.

HarmonyOS 2.0 inaonekana kwenda kwa kai na Huawei/Honor zipo kwenye msururu wa kuweza kuhamia kwenye toleo hilo jipya la programu endeshi.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] ambao wamekuwa wakipeleka programu endeshi ya kwao kwenye simu janja nyingi zaidi wanatazamiwa kufanya uzinduzi wa bidhaa mbalimbali mnamo Oktoba 21 […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania