fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Huawei Teknolojia

Huawei: Tarehe rasmi ya ujio wa HarmonyOS

Huawei: Tarehe rasmi ya ujio wa HarmonyOS

Spread the love

Huawei ambao wamekuwa wakisikika kuhusu programu yao endeshi kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Kampuni hiyo yenye makao yake makuu nchini Uchina imeweka wazi tarehe rasmi ya ujio wa HarmonyOS.

Habari kuhusu ujio wa HarmonyOS zimevuma kwa sana katika miezi ya karibuni lakini sasa tarehe rasmi ya ujio programu endeshi imewekwa wazi ambapo itafanyika hafla ya uzindunzi.

ujio wa HarmonyOS

Juni, 2 2021 ndio tarehe rasmi ya uzinduzi wa HarmonyOS.

Kitakachofanyika kwenye uzinduzi wa programu endeshi ya Huawei

SIku hiyo ya Juni 2 2021 pamoja na utambulisho wa programu endeshi pia simu janja MatePad Pro 2 na Huawei Watch 3 ambazo zote zitakuwa na hicho cha kwao wenyewe.

ujio wa HarmonyOS

Huawei MatePad Pro 2: Moja ya bidhaa za Huawwei smbazo zinatuma programu endeshi ya kwao wenyewe.

Baada ya uzinduzi wa HarmonyOS kuna simu janja ambazo zimewekwa kwenyw mpango wa kuruhusu wanazimiliki kuweza kushusha toleo hilo na kuanza kutumia’ kwa lugha rahisi kutoka kwenye Android na kuhamia HarmonyOS. Rununu ambazo zipo kwenye mpango ni Mate 40, Mate 40 Pro, Mate 40 Pro+, Mate 40 RS, Mate X2, Nova 8, Nova 8 Pro na MatePad Pro.

SOMA PIA  Kutojibu "sms" kwasababisha mume kupewa talaka!

Fununu zinasema HarmonyOS na Android ni kama mapacha wasiofanana kutokana na jinsi ambavyo inaonekana na hata vipengele vyake ndani lakini kwa sasa inatubidi tuwe wavumilivu hadi Juni 2 2021 tutakapoweza kufahamu kila kitu kinagaubaga.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] post Huawei: Tarehe rasmi ya ujio wa HarmonyOS appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania