Huawei ambayo mpaka sasa inapitia wakati mgumu wa kibiashara kutokana na vikwazo mbalimbali imeshauriwa kuweka nguvu zaidi kwenye utengenezaji wa programu wezeshi.
Dunia nzima inafahamu panda shuka ya Huawei kwenye biashara na soko la ushindano kwa ujumla wake kitu ambacho kimemuibua mwanzilidhi wa kampuni hiyo, Bw. Ren Zhengfei aliyeshauri ni vyema wakaweka nguvu ntingi kwenye utengenzaji wa programu wezeshi.
Huawei tangu mwaka 2019 wakati wa utawala wa rais Donald Trump imekuwa katika wakati mguu kutokana na kuwekewa vikwazo mbalimbali vya kufanya biashara kwa kile kiunachoaminika kuwa teknolojia yao si salama kwa raia jambo ambalo limefanya nchi mbalimbali kuweka nguvu kufanya nao biashara.
Huawei ipo kwenye orodha ya makampuni ambayo wananchi wa Marekani/mashirika ya nchini humo haytaruhusiwi kufanya nao biashara na kama ikifanyika basi ni kwa kibali maalum. Halikadhalika, teknolojia ya 5G wanayotoa Huawei haifanyi kazi kwenye nchi nyingi kutokana na kuelezwa kuwa ni hatari kwa matumizi.
Je, ni vita ya teknolojia ya 5G? Soma makala mengine kuhusu Huawei hapa – Teknokona/Huawei.
Mambo yanayoendelea Huawei
Tangu mwaka 2019, Huawei imekuwa ikitengenza programu endeshi ya kwao wenyewe (Harmony OS) ambapo intazamiwa katika siku za usoni tutaona simu janja kutoka kwao zikiwa na hicho walichokitengeneza wao wenyewe na hivyo kuachana na Android kimyakimya.
Hadi mwisho wa 2021 takribani simu janja milioni 300 za Huawei zinatumia programu endeshi yao wenyewe.
Hiyo ndio Huawei je, unafikiri inawabidi sasa wafikirie upande wa pili wa shilingi? Au bado wanapaswa kupigania ushindani wa kibiashara? Tupe maoni yako.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment