fbpx
simu, Smartphones, Teknolojia

Kampuni Ya Simu Janja, Vivo Kudhamini Kombe La Dunia!

kampuni-ya-simu-janja-vivo-kudhamini-kombe-la-dunia
Sambaza

Kampuni ya simu janja za Vivo inataka kujulikana duniani kote na kwa sasa imeweka wazi kuwa itakuwa inadhamini mashindano makubwa ya mpira wa miguu ya kombe la dunia.

Mpaka sasa kuna hati hati kubwa kuwa utakua hulijui kampuni hili la vivo lakini kama ushakanyaga china na baadhi ya sehemu za India utakuwa umeshakutana na simu hizi.

Kampuni Ya Simu Janja Za Vivo Kudhamini Kombe La Dunia

Vivo ni kampuni kubwa sana la simu huko china na linashindana na simu janja kubwa kama zile za Xiaomi na Oppo.

INAYOHUSIANA  Mambo 10 ya ujanja ujanja unayoweza kufanya kwenye iPhone 6/iPhone 6+

Kwa upande mwingine Vivo haina soko kubwa huko marekani na ulaya lakini kutokana na udhamini huu katika kombe la dunia ni wazi kuwa kampuni linataka kufahimika duniani kote.

Kingine cha kushangaza ni kwamba japokuwa kampuni hiyo haijulikani kwa sana lakini ni kwamba mpaka sasa ndio kampuni ya tano kwa ukubwa katika kutengeneza na kusambaza simu.

Chanzo cha takwimu hizi ni kutoka kwa IDC na wameangalia kigezo cha kusafirisha simu nyingi nje ya nchi.

Kampuni imetangaza kuwa imesaini mkataba wa miaka sita (2018 – 2022) na FIFA. Katika mkataba huo kampuni ndio litakuwa kampuni kubwa la simu kama mdhamini.

INAYOHUSIANA  Waathiriwa wa Samsung Galaxy Note 7 wabadilishiwa simu

Unaweza ukaona ni jinsi gani udhamini huo utakavyokuwa mkubwa kwa kuwa kwa takwimu tuu ni kwamba kombe la dunia ndio mashindano yanayotazamwa sana duniani kuliko mashindano mengine yoyote.

Kwa haraka haraka ni kwamba mashindano hayo yanapata uangalizi (views) mwingi sana. Kombe la dunia la mwaka 2014 lilipata uangalizi mara bilioni 3.2.

Huu sio udhamini wa kwanza mkubwa kutoka katika kampuni hilo. hata huko India kampuni limedhamini ligi kuu ya mpira baada ya pepsi kuachia ngazi. Jambo hili kwa namna moja ndio limelifanya kampuni kujulikana sana huko India.

INAYOHUSIANA  Ifahamu Smart Kicka kutoka Vodacom, Sifa Nzuri Kwa Bei Raisi

Vivo pia imesema kuwa ina mpango wa kutoa simu janja karibia na kombe la dunia spesheli kabisa kwa wapenda soka wote.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niambie ni nini unakiona kutoka katika kampuni baada ya kombe la dunia. Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com