fbpx

Motorola wametoa nyingine inaitwa Moto Z3

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

vodacom swahili

Sambaza

Ushindani wa kwenye soko la simu janja unaumiza kichwa makampuni mengi kiasi cha kwamba wanatoa simu baada ya simu. Wiki chache zilizopita tuliongelea kuhusu Moto Z3 Play lakini safari hii wametoa Moto Z3.

Motorola kwa maoni yangu naamini wanajaribu kujidhatiti kwenye soko ambalo kila kukicha kampuni zinajitahidi kushindana kwa kutoa simu/bidhaa ambazo zitapendwa na kuiletea sifa kampuni husika. Moto Z3 ni moja ya simu zenye nguvu kulingana na sababu zifuatazo:-

Kipuri mama (processor). Bila kukwepesha mambo Moto Z3 inatumia Snapdragon 835 SoC ikiwa ni moja ya vipuri ambavyo vina nguvu na uwezo wa kufanya simu ifanye kazi kwa ufanisi ulio bora zaidi.

Muonekano/Kioo. Kampuni ningi zinaonekana kuhama kwenye teknolojia kwa kioo chenye urefu wa ichi 5 na mambo ni vivyo hivyo kwenye Moto Z3 kwani ina urefu wa inchi 6 (uwiano wa 18:9).

wametoa

Kioo chake ni aina ya AMOLED ambacho chochote kinachoonekana kwenye kioo cha uang’avu wa hali ya juu sana.

Memori ya ndani/RAM. Moto Z3 imewekwa GB 64 na uwezo wa kukubali memori ya ziada mpaka TB 2. Kwenye upande wa RAM si haba kwani ina GB 4 ambapo suala zima la simu kukwamakwama kwa sababu ya kuzidiwa uwezo irakuwa nguvu.

INAYOHUSIANA  Samsung: Samsung Galaxy S10 ni familia ya simu nne! Fahamu vipya kutoka Samsung

Kamera/Betri. Kuna kamera mbili za nyuma na zote zikiwa na MP 12 na kamera ya mbele ina MP 8 ikiwa na imewekwa uwezo wa kutumia teknolojia ya kutambua sura ili kama njia mojawapo ya kuifanya simu kuwa salama. Betri la kwenye Moto Z3 lina 3000mAh ikiwa na teknolojia ya kuchaji simu kwa haraka.

wametoa

Kamera ndio kwa kiasi kikubwa inabeba uzuri wa simu janja sasa na Moto Z3 imesifiwa.

Mengineyo.

Moto Z3 imewekwa teknolojia ya kutumia alama ya kidole upande wa kulia pembezoni tofauti na simu nyingine ambazo zina aina hiyo ya ulinzi. Inatumia programu endeshi ya Android 8.1, inatumia 4G VoLTE, Wi-Fi 802.11 a/b/g/n/ac, Bluetooth v5.0, GPS/ A-GPS, NFC, and USB Type-C.

Moto Z3 ndio simu ya kwanza kuja na teknolojia ya 5G hivyo kasi ya intaneti kwenye simu hii itakuwa ni murua kwelikweli.

wametoa

Sehemu ambapo teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa na kwa hakika watu wengi hawajazoea muundo wa namna hiyo.

Simu hii sio nzito kwani ina uzito wa gramu 156 na bei yake $480|Tsh. 1,104,000 huku ikitazamiwa kuanza kuzwa duniani kote mwezi huu wa Agosti 2018.

Vyanzo: Gadgets 360, CNET

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.