BlackBerry Evolve na Evolve X zazinduliwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

BlackBerry ni moja kati ya makampuni ambayo yanaliangalia soko la simu nchini India kwa jicho la karibu sana kutokana na kwamba BlackBerry Evolve na Evolve X zimetengenezwa na Optiemus Infracom iliyo na leseni ya kutengeneza simu za BlackBerry nchini humo.

Uzinduzi wa simu hizo ulifanyika Agosti 2 2018 uliofanywa na kampuni ya Optiemus Infracom ambao ndio wamezitengeneza simu hizo kwa asilimia 100. Wahindi hawapendi simu za bei ghali na kutokana kwamba simu hiyo imetengenezwa nchini India basi bei yake haitakuwa ghali kutokana na kodi kwa bidhaa za ndani ipo chini.

Haina maana kuwa simu hizo hazina ubora ambao umezoeleka kwenye simu za BlackBerry la hasha! Kampuni hiyo imeweza kufuata vigezo vyote ambavyo kampuni mama iliwapa kwa ajili ya kutengeneza simu hizo. Sifa za simu zote mbili ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Micromax ya India Yaja na Simu Janja Nyembamba Zaidi Duniani

Muonekano/Kioo.Kwa muonekano tu safari hii wameamua kupumzisha kuweka kicharazio kinachoonekana; kwa maana ya kwamaba simu zote mbili ni za teknolojia ya kioo cha mguso. Simu zote mbizi zina kioo chnye urefu wa inchi 6 chochote kinachoonekana kwenye uso wa juu cha uang’avu wa juu (Full HD) aina ya LCD.

Kipuri endeshi (processsor). Hapa kuna utofauti kidogo kwani BlackBerry Evolve ina Snapdragon 450 SoC halafu BlackBerry Evolve X imewekwa Snapdragon 660 SoC. Kwa upande wa kipri kinachowezesha vitu vionekane ang’avu BlackBerry Evolve imewekwa Adreno 506 GPU huku Evolve X ikiwa na Adreno 512 GPU.

Evolve X

BlackBerry Evolve

RAM/Diski Uhifadhi. BlackBerry Evolve ina RAM ya GB 4, memori ya ndani ina GB 64 lakini ukiwa na uwezo wa kuweka memori ya ziada. BlackBerry Evolve X ina RAM GB 6 na GB 64 kwa upande wa diski uhifadhi pia uwezo wa kuweka memori ya zida mpaka TB 2.

INAYOHUSIANA  CES 2016: ThinkPad X1, Tableti ya Lenovo inayoweza kuwa Projector.

Kamera/Mfumo Endeshi. Simu zote mbili zina kamera mbili nyuma na moja mbele Kamera za nyuma zina MP 12 f/1.8+MP 13 f/2.6 (kwenye BlackBerry Evolve X) na ile ya mbele ina MP 16. BlackBerry Evolve ina MP 13 huku ya mbele ikiwa na MP 16.

Kamera ya kwenye BlackBerry Evolve X inaelezwa kuwa bora zaidi kuliko ile ya kwenye BlackBerry Evolve. Simu zote hizi zinatumia programu endeshi ya Android 8.1 Oreo.

Evolve X

BlackBerry Evolve X

Ulinzi. Kwa simu za BlackBerry hapa ndio huwa inafanya kampuni hiyo kupendwa. Simu zote mbili zina programu tumishi (DTEK) kwa ajili kuifanya simu hizo kuwa salama vilevile faragha. Pia simu hizo BlackBerry Hub ambapo mitandao ya kijamii, kipengele cha kupokea na kujibu jumbe vyote vipo kwenye BB Hub.

Betri/Mengineyo. Kwa simu zote mbili zina betri lenye 4000mAh pia zina teknolojia ya kuchaji bila kutumia waya. Sifa nyingine ni kama vile USB Type-C+OTG, ulinzi wa kutumia alama  ya kidole, 4G VoLTE, FM redio, sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ya ukubwa wa mm 3.5.

INAYOHUSIANA  China kujenga Kituo Kikubwa cha Utafiti chini ya Bahari

BlackBerry Evolve itaingia sokoni nchini India mwishoni mwa mwezi Septemba na bei yake ikiwa karibu $364|Tsh. 837,200 huku BlackBerry Evolve X ikielezwa kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi Agosti bei yake ikiwa ni $509|Tsh. 1,170,700.

Vyanzo: Android Authority, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.