fbpx
Intaneti, Kompyuta, simu, Teknolojia, Uchambuzi, Video

Downloading vs Streaming : Fahamu Tofauti Kuu, Kipi bora zaidi?

downloading-vs-streaming-fahamu-tofauti-kuu-kipi-bora-zaidi

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Mabadiliko ya kasi ya intaneti ndio yameleta vitu vingi ambavyo kwa wengine wanaweza wakawa hawajui maana ya maneno husika lakini kiuhalisia inawezekana kabisa akawa kwa namna moja au nyingine ameshawahi kuvitumia.

Downloading na Streaming ni maneno muhimu sana kufahamu maana yake kutokana na kwamba ukishajua yanamaanisha nini basi utaweza kuchagua kipi utachagua ili kuwea kufanikisha jambo fulani ukiwa unaperuzi mtandaoni.

Downlaoding na kwa tafsiri isiyo rasmi kupakua ni kitendo cha kuhifadhi kitu ambacho umekitoa mtandaoni kupitia simu, kompyuta au kifaa kingine chochote cha kidijitali.

Kitu ambacho kimeshushwa kutoka mtandaoni kinachukua sehemu ya memori kwenye kifaa husika; kama simu yako ina GB 32 kwenye memori ya ndani na kitu ambacho umekipakua kina ukubwa wa GB 2 basi simu husika itakuwa imebakiwa na GB 30 ambazo hazijatumika kwenye memori.

Downloading vs Streaming
Ukishapakuwa kitu maana yake utaweza kukiangalia muda wowote bila kuhitaji intaneti.

Streaming ni kitendo cha kuangalia picha jongefu mtandaoni bila mahitaji ya kukishusha ili uwe nacho kwenye kipakatalishi, simu, n.k kwa ajili ya kuangalia baadae. Mfano mzuri ni pale unapoangalia picha mnato mtandaoni mara baada ya kuisha/kuridhika na ulichokiona unaachana nacho na kuangalia kitu kingine.

Downloading vs Streaming
Katika miaka ya karibuni inaonekana watu wanapenda zaidi kuangalia vitu mtandaoni na kuviacha hukohuko.

Je, nini tofauti kati ya kupakua na kuangalia kitu mtandaoni?

Kupakua kitu ina maana itabidi usubiri kwa muda ili kuweza kuingia kwenye kifaa husika kutoka mtandaoni. Kuangalia kitu mtandaoni (streaming) hakuhitaji kusubiri kitu bali unaangalia wakati hapohapo.

INAYOHUSIANA  Xiaomi yauza simu Milioni 2 ktk Masaa 12, Rekodi ya Dunia ya Guinness Yawekwa

Kupakua kitu inahitaji simu/kompyuta iwe na nafasi (memori) ya kuweza kuhifadhi hicho ambacho unakishusha kutoka mtandaoni. Kuangalia kitu mtandaoni haihusiani kabisa na memori ya kifaa husika kwa sababu unakiangalia muda huohuo.

Kupakua kitu mtandaoni kunasababisha kutumia kiasi kikubwa cha intaneti ili kuweza kushusha kile ambacho unakitaka kuwa nacho kwenye kifaa cha kidijiti lakini ukiwa unaangalia vitu tu mtandaoni unaweza ukatumia kifurushi hicho kuangalia vitu vingi ukilinganisha kama ungekishusha kutoka mtandaoni.

Kipi bora kati ya kushusha/kuangalia tu mtandaoni?

Swali hili linaweza lisiwe na majibu ya moja kwa moja kutokana na vigezo mbalimbali kulingana mtu mwenyewe anavyopenda lakimi kitendo cha kuangalia kitu mtandaoni (streaming) kina maliza sana chaji si tu kwa sababu ya kuangalia tu lakini wakati huohuo inatumia intaneti kitu ambacho kinatumia sana nguvu ya betri.

Kwa upande mwingine kwanini utumie muda mrefu/mchache (kulingana na kasi ya intaneti) kusubiri mpaka kitu kimalizike ndio uweze kukiangalia wakati unaweza ukaangalia muda huohuo?.

Downloading vs Streaming
Watu wengi siku hizi wanapenda kuangalia vitu mtandaoni bila ya kuhitaji kuvipakua.

Hayo ndio mabadiliko ya teknolojia ambayo mwisho wa siku wewe ambae unaperuzi mtandaoni ndio utaweza kuamua uangalia tu au ukihifadhi kwenye kifaa kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Vyanzo: Quick & Dirty Tips, Lifewire

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|