Adobe ni kampuni namba moja duniani katika maswala ya kuhariri (ku’edit) picha kwani ina programu kabambe za kuliwezesha hilo.
Kampuni ya Adobe Inc inamiliki programu nyingi sana ambazo ni za simu na zingine ni za kwenye kompyuta.
Hivi karibuni imezindua App ya simu za iOs na Android ambayo inaitwa Adobe Scan. App hii inapatikana bure kabisa na lengo lake kubwa ni kumuwezesha mtumiaji kuweza mtumiaji kuweza ku’scan nyaraka zake
Utaweza hata ku’scan nyaraka zako na kuzihifidhi zikiwa katika mtindo maarufu wa pdf.
Nyaraka kama ‘Business card’, maandiko, picha, risiti n.k zinaweza kwa urahisi kabisa kuwekwa katika mfumo wa pdf na kuhifadhiwa kwa kutumia App hii.
Kingine cha tofauti ukifananisha na A[pp zingine ni kwamba Adobe Scan inauwezo wa kuhariri (edit) kabla huja’save kitu.
Tazama Video Hii Kujua Zaidi

Adobe Scan — Android
Adobe Scan — iOs