Kampuni ya Apple hivi sasa imetangaza upanuzi wa huduma zake kwa kuongeza upatikanaji katika nchi mbalimbali Duniani zikiwepo nyingi za afrika.
Kampuni hiyo imetangaza upatikanaji wa huduma maarufu kama vile duka la programu(App Store), Duka la games(Apple Arcade), Muziki wa Apple( Apple Music), Apple Podcasts na iCloud katika nchi zaidi ya 20 ambazo hazikuwepo kabla, na huduma mpya ya Apple Music inapatikana katika nchi zaidi ya 52.
Huduma za App Store, Apple Arcade, Apple Music, Apple Podcasts na iCloud sasa zinapatikana katika nchi na maeneo yafuatayo:
- Afrika: Kamerun, Cote d’Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon, Libya, Moroko, Rwanda, na Zambia.
- Asia-Pacific: Maldives na Myanmar.
- Ulaya: Bosnia na Herzegovina, Georgia, Kosovo, Montenegro, na Serbia.
- Mashariki ya Kati: Afghanistan (ukiondoa Muziki wa Apple) na Iraqi.
- Oceania: Nauru (isipokuwa Muziki wa Apple), Tonga, na Vanuatu.
Apple Music pia inaenea kwa nchi na maeneo yafuatayo:
- Afrika: Algeria, Angola, Benin, Chad, Liberia, Madagaska, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Namibia, Jamhuri ya Kongo, Senegal, Shelisheli, Sierra Leone, Tanzania, na Tunisia.
- Asia-Pacific: Bhutan.
- Ulaya: Kroatia, Iceland, na Makedonia ya Kaskazini.
- Amerika ya Kusini na Karibiani: Bahamas, Guyana, Jamaica, Montserrat, St Lucia, St Vincent na Grenadines, Suriname, Turks na Caicos, na Uruguay.
- Mashariki ya Kati: Kuwait, Qatar, na Yemen.
- Oceania: Visiwa vya Solomon
Zifahamu kwa uchache Huduma hizi tulizokuorodheshea ili kama baadhi huzitambui sasa uweze kuzijua kazi zake;
> APPLE STORE
App store ni program soko linalokusanya programu mbalimbali za bure na kulipia ambazo watumiaji wa vifaa vya apple huweza pakua programu zao wanazohitaji kwa urahisi. Kwa sasa inapatikakana katika nchi/mataifa 175 duniani kote na ndio duka la app linaloaminiwa sana kiusalama kuliko ata la Google Play Store . Ni mahali pazuri kwa watumiaji kugundua programu mpya na inaruhusu mtengenezaji yeyote kugawa programu zao kwa wateja ulimwenguni kote.
source: Apple
> APPLE MUSIC
Hii ni programu inayowezesha wateja wa Apple kutafuta na kusikiliza muziki . Apple Music ndio huduma bora zaidi ya muziki kwa iPhone, iPad, Apple Watch, Apple TV, Mac, HomePod, na CarPlay, na inapatikana pia kwenye vifaa vya Android na vifaa vingine.
source:Apple
> APPLE ARCHADE
Hii ni huduma inayopatikana ndani ya App Store inayomwezesha mteja kuweza kupakua programu za michezo na kucheza.Michezo iyo inayoweza kuchezwa kwa iPhone, iPad, iPod touch, Mac, na Apple TV. Apple Arcade inaongeza michezo mpya na matandazo kila mwezi kutoka kwa watengenezaji wa mchezo wa maono zaidi wa ulimwengu.
source : Apple
> APPLE PODCAST
Hii ni app na programu inaokusanya vipindi vya mfumo wa maongezi vinavyopatikana mtandaoni kwa mfumo wa podcast. Kwa mfano unaweza sikiliza vipindi vinavofanana na vya redio kupitia programu hii, na app za podcast zimekuwa maarufu hivi karibuni huku kukiwa na wafuatiliaji wengi sana. Kufahamu zaidi kuhusu Podcast soma makala yetu – Podcast ni nini?
Source : Apple
> ICLOUD
Hii ni huduma inayotoa nafasi ya kuhifadhi taarifa na data za mteja katika intaneti na kumfanya kuwa salama pindi hatumiapo kifaa chake cha Apple. Inaruhusu kuhifadhi picha, kuweka hati muhimu mikononi na kurahisisha kusambaza kwa marafika kwa usalama. Pia icloud inatumika kutafuta simu zilizopeta na kwa sasa takribani Nchi na mikoa 175. iCloud inakuja na 5GB ya uhifadhi wa bure na inatoa huduma iyo kwa uwezo wa nafasi za juu kama wa 50GB, 200GB, na 2TB kwa bei Nafuu. Hii inapatikana kwa watumiaji wa Mac, iPhone, iPad na kwenye Windows.