Tuliandika mengi kuhusu roboti-mbwa anayetengenezwa na kampuni ya Boston Dynamics. Kampuni ya Boston Dyanamics ishawahi kumilikiwa na Google kwa miaka mingi (2013 – 2017) kabla ya kuuzwa mwaka mwaka 2007 kwenda kwa shirika la SoftBank Group la nchini Japani.
Moja ya bidhaa yake maarufu kwa sasa ni roboti-mbwa anayetambulika kwa jina la Spot. Roboti huyo tayari alishaanza kuwa maarufu na kuuzwa kwa makampuni kwa ajili ya matumizi ya kama vile ubebaji mizigo kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kupitia eneo la mgongo wa roboti huyu basi anaweza kubadilishiwa matumizi kwa kupachikwa kifaa chochote kinachoendana na kazi ambayo unataka afanye.

Mfano ameshatumiwa katika hospitali mbili huko Marekani katika kipindi hichi cha Corona kuepusha mikutano isiyokuwa ya kilazima kati ya wahudumu wa afya na watu wanaokuja kwa ajili ya kupata huduma za afya ambazo si lazima kuwakutanisha kwa ukaribu kati ya mtoa huduma na mtu husika. Nchini Singapore polisi waliweka kamera kwenye roboti hawa na kuwatumia kuzunguka maeneo ya bustani za jamii kuhakikisha watu wanaotembelea maeneo hayo wanafuata utaratibu wa usalama dhidi ya COVID-19/Corona.
Na sasa kwa mara ya kwanza mtu yeyote anaweza kununua roboti huyu. Ila tatizo bei.
Bei ya roboti huyo inaanzia dola 74,500 za Marekani. Hii ni zaidi ya milioni 150 za Kitanzania kwa roboti mmoja.
Kuna makampuni yanayowatumia roboti hawa katika kazi za uangaliaji/uchunguzi wa maeneo (survey), hasa hasa maeneo ambayo yanaweza kuwaweka binadamu kwenye hatari za sumu au hatari zingine kama hizo.
Kutokana na bei yake tusitegemee kuona watu wakinunua roboti hawa kwa ajili ya kuchezea. Ila kama teknolojia zingine zilivyo, ina aminika bei za roboti wa namna hii zitaendelea kushuka miaka inavyozidi kwenda mbele.
Je una mtazamo gani juu ya utumiaji wa roboti hawa?
Soma pia:
- Roboti Mbwa aanza kupatikana, ukimuhitaji andaa bei ya gari jipya
- Habari mbalimbali za sekta ya roboti – Teknokona/Roboti